PID
• • • • •
PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)
PID NI NINI?
PID ni maambukizi ya Bacteria kwenye via vya Uzazi vya mwanamke, ambapo hicho ni kifupi cha Maneno haya"Pelvic inflammatory Disease"
TATIZO HILI LINA DALILI ZIPI?
Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za Ugonjwa wa PID kwa Wanawake;
- Mwanamke Kupata maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu
- Mwanamke kutoa damu wakati na baada ya tendo la Ndoa
- Mwanamke kutoa uchafu wenye rangi kama ya njano n.k
- Mwanamke kutoa uchafu wenye harufu mbaya ukeni
- Kutoa maji maji sehemu za siri mara kwa mara
- Mwanamke kublid katikati ya mwezi
- Mwanamke kupata maumivu makali wakati wa tendo la Ndoa
- Joto la mwili kupanda au mgonjwa kuwa na homa
- Pia kwa baadhi ya wanawake hupata maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, na kupata shida ya kutoa mkojo
N.k
CHANZO CHA TATIZO LA PID
Ugonjwa wa PID husababishwa na BACTERIA ila magonjwa kama Gonorrhea pamoja na Chlamydia huchangia sana uwepo wa Tatizo hili
MATIBABU YA UGONJWA WA PID
- Ugonjwa huu au tatizo hili la PID hutibiwa kwa dawa mbali mbali kama vile; Doxcycline n.k
Na matibabu haya ni vizuri kufanyika kwa mwanamke pamoja na mwanaume ambaye anashiriki naye tendo la ndoa,ili kuepusha tatizo kujirudia tena.
mwanamke mwenye tatizo la PID hushauriwa kutokufanya mapenzi mpaka apone.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!