SABABU ZA MTU KUPIGA MIAYO(Kwa kitaalam yawning)

 MIAYO

• • • • • •

SABABU ZA MTU KUPIGA MIAYO(Kwa kitaalam yawning)


Hakuna mtu ambaye hajawahi kupiga miayo, lakini swali ni je hivi kupiga miayo husababishwa na nini?


Katika makala hii,nakuonyesha baadhi ya sababu kuu za mtu kupiga miayo


SABABU ZA MTU KUPIGA MIAYO(Kwa kitaalam yawning)


Zipo sababu mbali mbali ambazo husababisha mtu kupiga miayo na sababu hizo ni kama vile;


✓ Mtu kupata uchovu wa mwili sana kutokana na kazi nyingi,ngumu n.k


✓ Mtu kuwa na tatizo la usingizi


✓ Matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; dawa za tatizo la msongo wa mawazo,hofu au anxiety n.k


✓ Lakini pia kwa uchache, kupiga miayo sana mfululizo huweza kuwapata watu wenye matatizo mbali mbali kama vile;


- Tatizo la damu kuvuja ndani ya moyo


- Watu wenye tatizo la shambulio la moyo


- Watu wenye tatizo la uvimbe kwenye ubongo yaani Brain tumor


- Watu wenye tatizo la kifafa au epilepsy


- Watu wenye tatizo la mwili kushindwa kudhibiti kiwango cha joto mwilini


- Watu wenye tatizo la Ini kushindwa kufanya kazi

N.k


ZINGATIA HAYA KUKUSAIDIA;


• muda mzuri wa kulala


• fanya mazoezi ya mwili kila siku


• epuka matumizi ya dawa hovio



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!