SABABU ZA VIDONDA VYA MGONJWA WA KISUKARI KUCHELEWA KUPONA(au mgonjwa kukatwa kabsa viungo)
KISUKARI
• • • • •
SABABU ZA VIDONDA VYA MGONJWA WA KISUKARI KUCHELEWA KUPONA(au mgonjwa kukatwa kabsa viungo)
Kitendo cha mtu kuwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko kawaida huleta madhara mbali mbali ikiwa ni pamoja na vidonda kutokupona haraka, mtu kukatwa viungo kama miguu n.k
SABABU ZA VIDONDA VYA MGONJWA WA KISUKARI KUCHELEWA KUPONA(au mgonjwa kukatwa kabsa viungo)
- Kuwa na kiwango kikubwa cha sukari mwilini;
• huzuia virutubisho pamoja na hewa ya oxygen kufika na kusaidia seli hali ambayo husababisha seli zizidi kufa, na zile ambazo tayari zimekufa zishindwe kufanyiwa repair hali ambayo hupelekea vidonda kuchelewa sana kupona au kutokupona kabsa
• Kiwango kikubwa cha sukari mwilini huzuia kinga yako ya mwili kutokufanya kazi vizuri
• Ongezeko la sukari huvutia sana vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile bacteria na kusababisha sehemu ya kidonda kuzidi kushambuliwa kwa kasi zaidi, kwani wadudu hawa hufata sukari
• Kiwango kikubwa cha sukari huongeza tatizo la seli za mwili kuvimba
• Tatizo la sukari kuwa juu kuliko kawaida husababisha Kuwe na mzunguko mbaya wa damu kwenye seli za mwili
• Kuwa na shida ya kuharibika kwa mfumo wa fahamu au nerves
N.k
KUMBUKA; endapo vidonda hivi visipotibiwa vizuri kwa haraka na kiwango cha sukari mwilini kuzibitiwa hali ya vidonda huweza kuwa mbaya zaidi na wengine hadi kufikia hatua ya kukatwa viungo
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!