SARATANI YA ZIWA KWA WANAUME

   KANSA

• • • • •

SARATANI YA ZIWA KWA WANAUME


Asilimia kubwa ya watu hawajui kwamba kuna saratani ya ziwa kwa wanaume,wengi wao wanajua kwamba kuna saratani ya matiti kwa wanawake tu.


Ila ukweli ni kwamba,hata wanaume huweza kupatwa na aina hii ya saratani japo namba yao sio kubwa kama wanawake.


CHANZO CHA SARATANI HII KWA WANAUME


- Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo hujulikana kama chanzo cha saratani hii japo kuna baadhi ya vitu ambavyo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata aina hii ya saratani kama vile;


✓ Umri kuwa mkubwa


✓ Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huhusisha kuongeza vichocheo vya mwilini kwa muda mrefu


✓ Kuwa na historia ya tatizo hili katika famili yenu


✓ Mwanaume kufanyiwa upasuaji wa korodani


✓ Unene kupita kiasi

N.K


DALILI ZA SARATANI HII NI PAMOJA NA;


- Mwanaume kupata maumivu makali kwenye ziwa


- Mwanaume kuanza kutoa usaha au damu kwenye ziwa


- Ziwa moja kuanza kuwa kubwa kuliko lingine


- Sehemu ya ziwa kubadilika rangi na kuwa nyekundu sana


- N.K


MATIBABU YA TATIZO HILI


-Mojawapo ya matibabu ya kansa hii ni pamoja na mgonjwa kufanyiwa upasuaji, huduma ya Chemotherapy, dawa za vichocheo mwilini, huduma ya mionzi(Radiation therapy) N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!