TATIZO LA FANGASI WA KWENYE UBONGO(chanzo,dalili na tiba)

   FANGASI

• • • • •

TATIZO LA FANGASI WA KWENYE UBONGO(chanzo,dalili na tiba)


Mashambulizi ya fangasi kwenye mwili wa binadamu huhusisha maeneo mbali mbali kama vile, kichwani, kwenye ulimi,mdomoni,kwenye damu,sehemu za siri,miguuni,mikononi n.k


Leo tunazungumzia kuhusu mashambulizi ya fangasi wa kwenye ubongo ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Mucormycosis. Moja ya mashambulizi ya Fangasi ya hatari na ambayo hupoteza maisha ya watu wengi.


DALILI ZA TATIZO LA FANGASI WA UBONGO NI PAMOJA NA;


- Mtu kupata maumivu makali ya kichwa upande mmoja


- Mtu kupata uvimbe wa rangi nyekundu machoni


- Mtu kupata shida sana ya upumuaji


- Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa


- Mgonjwa kutokwa na kamasi puani ambalo lina rangi nyeusi


- Mwili kuchoka sana kupita kawaida


- Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya kula chakula


- Uzito wa mwili kuanza kushuka kwa kasi


- Rangi ya ngozi kwa mgonjwa kubadilika na kuanza kuwa nyekundu kisha baadae weusi huingia.


- Mgonjwa kupatwa na hali ya kukohoa mara kwa mara

n.k


MATIBABU  YA TATIZO HILI


- Fangasi hawa hutibiwa kwa dawa mbali mbali za Fangasi ikiwa zile ambazo hupitishwa kwa Njia ya Mshipa yaani Intravenous(IV)fungal Drugs pamoja na Njia ya upasuaji wa ubongo kwa ajili ya kuondoa Tissu zilizoathiriwa na fangasi hawa.


KUMBUKA; haya ni miongoni mwa mashambulizi ya Fangasi ambayo hutokea kwa nadra sana lakini ni hatari sana, huweza kusababisha mtu kupoteza maisha ndani ya muda mfupi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!