Ticker

6/recent/ticker-posts

Tatizo la Kuvuja Damu kwenye mfumo wa Chakula(CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE)



 DAMU

• • • • •

Tatizo la Kuvuja Damu kwenye mfumo wa Chakula(CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE)


Hapa tunazungumzia mtu kuvuja damu kwenye eneo lolote lile ndani ya mfumo mzima wa chakula yaani Kuanzia Mdomoni mpaka kwenye Njia ya haja kubwa(anus).


CHANZO CHA TATIZO HILI


- zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kupatwa na tatizo la kuvuja damu kwenye eneo lolote lile ndani ya mfumo mzima wa chakula kama vile;


✓ Mtu kuwa na tatizo la uvimbe


✓ Mtu kuwa na tatizo la vidonda vya tumbo yaani peptic Ulcer


✓ Mtu kuwa na kitu kama pochi au bag kwenye mfumo wa chakula


✓ Kuvimba kwa Njia ya chakula


✓ kutanuka na kuongezeka ukubwa kwa mishipa ya Veins ndani ya njia ya chakula


✓ Kupata jeraha au michubuko yoyote kwenye njia ya chakula


✓ Tatizo la kansa au saratani kwenye maeneo mbali mbali ya mfumo wa chakula


✓ Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria,Fangasi au Virusi


n.k


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


• Mtu kujisaidia kinyesi kilichochanganyika na damu au chenye rangi nyeusi


• Mtu kutapika matapishi ambayo yamechanganyika na damu, yenye rangi nyekundu au Dark brown


• Mtu kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa


• Pamoja na dalili nyingine jumuishi kama vile;


- Kushuka kwa shinikizo la damu au Presha


- Mapigo ya moyo kwenda mbio


- Mtu kupoteza fahamu


- Mtu kutokupata mkojo kabsa au kukojoa mkojo mdogo sana


- Kupata maumivu ya tumbo


- Kupata maumivu ya kifua


- N.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


- Tatizo hili la kuvuja damu kwenye maeneo mbali mbali ndani ya mfumo mzima wa chakula hupona lenyewe, 


Japo pia mtu huweza kupata matibabu kama hali ni mbaya zaidi kulingana na chanzo husika 


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments