Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA KUWA ALBINO AU ZERUZERU(chanzo)



 ALBINO

• • • • • •

TATIZO LA KUWA ALBINO AU ZERUZERU(chanzo)


Tatizo la kuwa Albino au kwa jina lingine zeruzeru ni ulemavu wa ngozi ambao husababishwa na upungufu au ukosefu wa pigment inayojulikana kama Melanin,


Melanin ndyo hufanya kazi ya kuipa ngozi ya mwili rangi yake,hivo endapo itapungua au kukosekana kabsa ndipo tatizo la ualbino hutokea,


 lakini pia tatizo hili huhusishwa na maswala ya genetics katika familia au koo flani.


Mbali na tatizo hili la kwenye ngozi,watu ambao ni Albino hupatwa na tatizo la kutokuona vizuri pamoja na ngozi yao kuharibiwa sana na miale ya jua.


Hivo basi;


MADHARA YA TATIZO LA UALBINO NI PAMOJA NA;


- Mtu kubadilika rangi ya ngozi pamoja na nywele


- Mtu kupatwa na matatizo ya kutokuona vizuri


- Mtu kuharibiwa ngozi yake ya mwili na miale ya jua au baada ya kuchomwa na jua,


ngozi kubadilika na kuwa nyekundu zaidi, kuwa na vitu vyeusi vyeusi kwenye ngozi n.k


MATIBABU YA TATIZO LA KUWA ALBINO


- Tatizo hili halina tiba,bali mtu mwenye tatizo hili hufanya mambo mbali mbali yakumsaidia ili asipate madhara zaidi kama vile;


✓ Kuvaa kofia wakati wa jua kali


✓ Kuvaa nguo ndefu wakati wa jua kali


✓ Kufanya vipimo vya macho mara kwa mara

n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments