AFYA KWA MTOTO
• • • • • •
TATIZO LA MTOTO KUTOKULIA BAADA YA KUZALIWA
Nidhahiri kwamba umewahi kusikia kwamba mtoto mara tu baada ya kuzaliwa anatakiwa alie,asipolia watu huanza kuhisi kuna tatizo, je hii ipoje?
Ni kweli hata wataalam wa afya wakati wanamzalisha mama, baada ya mtoto kutoka tu hufurahi sana akilia, Kulia kwa mtoto mara tu baada ya kuzaliwa ni kiashiria kwamba mtoto yupo vizuri ikiwa ni pamoja na mapafu yake yanafanya kazi vizuri,
Hivo mtoto kutokulia huweza kuwa ni shida kwenye mapafu, njia ya hewa kuziba,mtoto kunywa maji ya uzazi n.k, JAPO sio kila mtoto ambaye baada ya kuzaliwa hajalia anashida.
Zipo njia mbali mbali ambazo wataalam wa afya huweza kuzitumia ili mtoto alie, kama vile; Kumsugua mgongoni, kutoa uchafu puani na mdomoni N.k,
Endapo baada ya juhudi hizi zote bado mtoto hajalia, Mtoto huyu huwekwa chini ya uangalizi maalum na kuanza uchunguzi zaidi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!