UVIMBE
• • • • • •
TATIZO LA MTU KUPATA UVIMBE KWENYE TEZI LA MATE(salivary gland tumor)
Tatizo hili huhusisha ukuaji wa seli usio wakawaida katika eneo la Tezi la mate yaani Salivary gland hali ambayo hupelekea tezi kuvimba na kuongezeka ukubwa.
DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
✓ Mtu kuonekana kuvimba eneo la mashavuni au kwenye taya
✓ Mtu kuhisi hali ya kuchomwa chomwa usoni
✓ Mtu kupata shida ya kufungua mdomo
✓ Mtu kupata shida ya kumeza kitu chochote
✓ Misuli ya upande mmoja wa shavu kulegea
✓ Mtu kupata maumivu makali eneo la tezi la mate
n.k
CHANZO CHA TATIZO HILI
- Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo imehusishwa na kusababisha tatizo hili, japo imeonekana baadhi ya watu wapo kwenye hatari ya kupata shida hii kama vile;
• Wazee
• Watu ambao wanapata huduma ya mionzi yaani Radiation therapy
• Watu ambao hufanya kazi kwenye madini
• Watu ambao hufanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza mipira(rubber)
N.k
MATIBABU YA TATIZO HILI
- matibabu ya tatizo hili ni pamoja na Mgonjwa kufanyiwa upasuaji, Kupata huduma ya Chemotherapy, radiotherapy pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali kama za maumivu N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!