azoospermia
• • • • •
TATIZO LA MWANAUME KUTOKUWA NA MBEGU ZA KIUME KABSA(azoospermia)
Azoospermia ni tatizo la mwanaume kukosa mbegu za kiume kabsa, kwa tafsri nyingine, hakuna mbegu zozote zinazozalishwa au kupitishwa kwa mwanaume mwenye tatizo hili, hapa nitofautishe na tatizo la Low sperm count,
Low sperm count ni tatizo la mwanaume kuwa na mbegu chache au chini ya kiwango kinachotakiwa, lakini kwa mwanaume mwenye tatizo la Azoospermia hana mbegu za kiume kabsa.
•Soma: Sababu za Mwanaume kushindwa Kumpa Mwanamke Mimba
CHANZO CHA TATIZO LA MWANAUME KUKOSA MBEGU ZA KIUME(AZOOSPERMIA)
- Kuziba kwa Mirija ya kupitisha mbegu za kiume kutokana na sababu mbali mbali kama vile;
• Kuumia au ajali
• maambukizi ya magonjwa mbali mbali
• uvimbe kwenye mirija ya kupitisha mbegu
• upasuaji ambao umefanyika kwenye maeneo haya ya mirija
n.k
- Sababu nyingine ni matatizo ya Kigenetics kwa baadhi ya wanaume, mfano;
Tatizo ambalo hujulikana kama Klinefelter’s syndrome, ambapo mwanaume hubeba kiwango cha chromosome X kilochozidi hivo badala ya kuwa na XY kama wanaume wengine, mwanaume huyu huwa na XXY,
tatizo hili hupelekea hata mwanaume kushindwa kumpa mimba mwanamke
- Matatizo ya mvurugiko wa vichocheo mwilini yaani Hormone imbalance au endocrine disorders,
Mfano; Tatizo la hypogonadotropic hypogonadism hyperprolactinemia na androgen resistance
- Matatizo mbali mbali ambayo huhusisha korodani kama vile;
mwanaume kukosa korodani, korodani kutokushuka chini kwenye vifuko vyake(scrotum) yaani kwa kitaalam cyptorchidism n.k
- Matatizo yahayohusu umwagaji wa mbegu za kiume,
•Soma: Sababu za Mwanaume kushindwa Kumpa Mwanamke Mimba
Mfano; tatizo la Retrograde ejaculation, ambapo mwanaume humwaga mbegu za kiume kuelekea kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuzitoa nje
MATIBABU YA TATIZO HILI
- Tatizo hili la mwanaume kukosa mbegu za kiume hutibiwa kwa njia mbali mbali kulingana na chanzo chake,
ila kwa ujumla wake matibabu huweza kuhusisha dawa mbali mbali kama vile; dawa za kubalance hormones, dawa za kuondoa uvimbe n.k Pamoja na huduma ya upasuaji kwa mgonjwa
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!