TATIZO LA TUNDU LA MKOJO KWA MWANAUME KUWA CHINI BADALA YA MBELE kwenye Uume(Hypospadias)

 hypospadias

• • • • •

TATIZO LA TUNDU LA MKOJO KWA MWANAUME KUWA CHINI BADALA YA MBELE kwenye Uume(Hypospadias)


Tatizo la tundu la mkojo kwa mwanaume kuwa chini badala ya mbele kwenye Uume ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Hypospadias, huweza kugundulika baada ya mtoto kuzaliwa, na wakati wa kukojoa.


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA


- mwanaume kuonekana kuwa na tundu la mkojo kwa chini ya uume badala ya mbele


- Mwanamke kukojoa na mkojo kutokea kwa chini


- Uume kupinda kuelekea chini

n.k


CHANZO CHA TATIZO HILI


- Tatizo hili hutokea wakati wa uumbaji wa mtoto, ambapo hitilafu huhusisha vichocheo au hormones zinazohusika na urekebishaji wa njia ya mkojo yaani Urethral pamoja na ngozi ya mbele foreskin.


WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA SHIDA HII


✓ Kuwa katika familia au koo ambapo kuna mtu aliyepatwa na tatizo hili


✓ Mama kubeba mimba akiwa na umri wa zaidi ya miaka 35


✓ Mama mjamzito kula sumu,kemikali au dawa zozote ambazo huweza kuathiri uumbaji wa mtoto na kusababisha hali ya ulemavu


MATIBABU YA TATIZO HILI


- Huhusisha njia ya upasuaji ambapo mwanaume hufanyiwa upasuaji na kurekebishwa shida hii.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!