TATIZO LA VIDONDA PAMOJA NA NGOZI KUCHUBUKA KWA WAGONJWA(bedsores)
AFYA TIPS KWA WAGONJWA
• • • • •
TATIZO LA VIDONDA PAMOJA NA NGOZI KUCHUBUKA KWA WAGONJWA(bedsores)
Tatizo la ngozi kuchubuka pamoja na vidonda hutokea sana kwa wagonjwa ambao hawajiwezi,hivo kupelekea kukaa au kulala kwa muda mrefu mpaka atokee mtu wakuwabadilisha upande wa kulala.
Tatizo hili hujulikana kama Bedsores na husababishwa na sababu mbali mbali kama vile;
- Msuguano kwenye ngozi katika eneo flani
- Mgandamizo wa muda mrefu n.k
ENEO AMBALO HUATHIRIWA SANA NA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
- Sehemu ya matakoni
- Sehemu ya mgongoni
- Sehemu ya begani kwa nyuma
- Sehemu ya nyuma ya mkono au mguu
DALILI ZA KUTOKEA KWA TATIZO HILI Kwenye eneo ambalo Mgonjwa huweza kuchubuka ngozi au kupata kidonda(Bedsores)
✓ Ngozi ya eneo hilo kuanza kubadilika rangi pamoja na muonekano wake(texture)
✓ Sehemu hiyo kuanza kuvimba
✓ Kuanza kutoa maji maji kama usaha
✓ Sehemu hyo kuwa na joto zaidi au baridi zaidi kuliko maeneo mengine ya mwili
✓ Kuanza kuhisi maumivu kwenye eneo husika, au kuhisi kufa ganzi kwenye eneo husika n.k
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA MGONJWA
- Hakikisha mgonjwa kama huyu halali upande au sehemu moja kwa muda mrefu,abadilishwe upande mara kwa mara
- Hakikisha ngozi ya mgonjwa inakuwa safi na kuepuka ukavu muda wote,hivo apakwe mafuta kwenye ngozi mara kwa mara
- Mgonjwa ale vyakula ambavyo vina virutubisho muhimu kama proteins,vitamins N.k
- Mgonjwa anywe maji ya kutosha pamoja na kula vyakula na matunda ambayo yana kiwango kikubwa cha maji
- Mgonjwa asiwe anavuta kabsa Sigara
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!