Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA VIRIBATUMBO KWA WATOTO



VIRIBATUMBO

• • • • • •

TATIZO LA VIRIBATUMBO KWA WATOTO


Kwa wazazi wote ,kumekua na ongezeko kubwa sana la Watoto wenye viribatumbo na hasa hasa Watoto wa wazazi waishio mijini..


Kwa tafiti zilizofanywa katika maeneo mengi ulimwenguni zinaoyesha kwamba Pamoja na ULAJI WA HOVYO USIOFUATA UTARATIBU WA MPANGILIO MZURI WA AFYA, KUMEKUA NA ONGEZEKO LA MATUMIZI YA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI KAMA SIMU, KOMPYUTA ZA WATOTO, KUANGALIA KATUNI NA GAME KWENYE TV NK. KUMEKUA NA ONGEZEKO KUBWA LA WATOTO KUTOKUA NA AFYA NJEMA NA BADALA YAKE WAMEKUA WANANENEPA NA KUPATA VIRIBATUMBO (CHILDHOOD OBESITY)


Natoa wito kwa wazazi kutowapa SIMU Watoto kwa ajili ya kuangalia katuni au kucheza gemu,kutokuwaacha Watoto wakae kae kwenye TV na badala yake wawe wanacheza michezo ya kusismua mwili au kufanya kazi zingine,kutokuwapa vifaa vya kielektroniki kama laptop kwani zinadumaza na kuwafanya wawe vibonge


Najua wazazi wengi mnaniangalia kwa mshangao ila ni jukumu langu kuwaambia ukweli


Najua wazazi wengi hufurahia wanapoona mtoto wao ni kibonge bonge jambo ambalo kiafya ni hatari sana kwa maisha ya mtoto baadae, mtoto anakua kwenye hatari ya kupata magonjwa ya moyo,kisukari,presha,kuzeeka haraka ingali bado mtoto.


Nitoe ushuhuda nilishawahi kumuambia mtoto mmoja wa kike shkamoo dada nikashangaa nae ananiambia shikamoo baba,nilipouliza umri wake mama yake kaniambia ana miaka 11,alikua na maka 11 ila allikua mkubwa sana na anaonekana kama mtu mwenye miaka 40.. hatari sana. cc.Dr.mathew






Post a Comment

0 Comments