UFAHAMU UGONJWA WA "NARCISSISTIC PERSONALITY DISORDER".
AFYA TIPS
• • • • •
UFAHAMU UGONJWA WA "NARCISSISTIC PERSONALITY DISORDER".
By Dr.Christopher Cyrilo (MD)
Umewahi kusikia ugonjwa wa akili uitwao 'Narcissistic personality disorder (NPD).?' Huenda hujawahi kusikia jina hilo lakini pengine umewahi kuona mtu mwenye dalili za ugonjwa huo. Kadri utakavyoendelea kusoma utaweza kuoanisha dalili za ugonjwa huu na jamii unayoishi nayo na kuona kati ya jamaa zako kama kuna yeyote anayeugua gonjwa hili hatari la akili.
Ugonjwa huu huwaathiri sana watu wazima na hususani viongozi wa taasisi mbalimbali lakini zaidi taasisi za kisiasa. Wapo baadhi ya viongozi wa taasisi nyingine kama vile za dini, elimu, mashirika, makampuni ambao huweza kuugua pia lakini wahanga wakubwa wa ugonjwa huu ni viongozi wa kisiasa.
DALILI ZAKE:
1. Dalili mojawapo za gonjwa hili ni kuwa mtu wa kujisifu na kujivuna (self centered and egoistic), kupaniki, kudharau wengine na kupuuza hisia zao.
2. Mgonjwa huhisi kuwa yeye tu ndio mtu muhimu kuliko wengine na mawazo yake ni sahihi kuliko mawazo ya wengine, na hakuna mjadala.
3. Maneno na vitendo vya wagonjwa wa Narcissistic Disorder hulenga tu kwenye kujijengea umaarufu na mafanikio binafsi na kutaka kupendwa na watu.
4. Wagonjwa hawa wanapokuwa viongozi, hutumia zaidi vyombo/watu wanaomuunga mkono kukandamiza watu wasiomuunga mkono.
5. Wagonjwa wa aina hii huchagua maneno ya vitisho na mbinu za kuogofya ili kujipa nafasi ya kutamba katika ulingo wa siasa bila changamoto kutoka kwa wapinzani wake.
Mifano ya viongozi wa aina hii ni Idd Amin Dada wa Uganda na Adolf Hitler wa Germany. Na hao pia walikuwa na wafuasi wengi pamoja na matendo yao yasio ya kawaida.
ATHARI ZAKE:
Wataalamu wa saikolojia wanashauri kuwa, wagonjwa wa "Narcissistic personality disorder" hawapaswi kuwa viongozi wakubwa wa kisiasa. Wanafaa kuongoza familia, kampuni, vikao vya ukoo au jumuiya ndogondogo ambapo watu ni wachache na mawazo kinzani ni nadra.
Lakini wanapopewa majukumu ya kuongoza mataifa/nchi au taasisi kubwa ambapo watu ni wengi na kuna mawazo mengi kinzani huweza kuleta maafa makubwa sana ikiwemo umwagaji wa damu.
Mbaya zaidi, watu wenye gonjwa hili huweza kujiona watakatifu, wapenda watu na watu wazuri, tofauti na matendo yao.
MATIBABU:
Matibabu ya ugonjwa huu ni magumu sana kwa sababu mgonjwa huwa hajui kama anaumwa, na hata ukiambiwa huwa hakubali. Wengi wanaougua ugonjwa huu ukiwaambia wao ni wagonjwa wanaweza kukuadhibu.
Wagonjwa wa aina hii hupatiwa matibabu maalumu ya mazoezi ya akili (psychotherapy) kutoka ka wataalamu waliobobea (Psychotherapist). Hakuna dawa mahususi ya kumeza kwa wagonjwa wa aina hii, lakini kama hali itakua mbaya wanaweza kutibiwa kwa kutumia #antidepressants au #antianxiety.
SWALI;
Je, katika jamii yako unayoishi umewahi kuona dalili za kuongozwa na mtu mwenye ugonjwa huu wa akili? Je umechukua hatua gani??
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!