UGONJWA UNAOTOKANA NA HUDUMA YA MIONZI(Radiation Sickness)

 MIONZI

• • • •

UGONJWA UNAOTOKANA NA HUDUMA YA MIONZI(Radiation Sickness)


Huduma ya mionzi yaani radiotherapy hutolewa kwa wagonjwa mbali mbali Wa Kansa au Saratani za aina mbali mbali,


Lakini endapo mtu atapata mionzi kwa kiasi kikubwa sana ndani ya muda mfupi huweza kuharibu kabsa mwili wake na kusababisha tatizo ambalo hujulikana kwa kitaalam kama Radiation Sickness.


DALILI ZA MTU ALIYEATHIRIWA NA MIONZI MWILINI


- dalili hutegemea wingi,ukubwa au Nguvu ya mionzi ambayo mtu kapata, Lakini kwa ujumla wake zipo dalili mbali mbali kama vile;


✓ Mtu kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika


✓ Mtu kupata maumivu makali ya kichwa


✓ Mwili kukosa nguvu kabsa


✓ Mtu kuanza kuharisha


✓ Mtu kuanza kupata kizunguzungu kikali


✓ Nywele kuanza kunyonyoka na kukatika zenyewe


✓ Mtu kupata homa au joto la mwili kupanda sana


✓ Presha ya mwili kushuka gafla na kuwa chini


✓ Mtu kutapika Damu

N.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


- Matibabu ya tatizo hili huhusisha njia mbali mbali kama vile;


• Kurepair viungo au mifupa iliyoathiriwa na mionzi


• Kufanya huduma inayojulikana kama Decontamination, kwa ajili ya kuondoa baadhi ya particles za mionzi zilizopo nje


• Pamoja na dawa mbali mbali za kudhibithi dalili kama vile;


- Kichwa kuuma sana


- Kuharisha


- Kichefuchefu na kutapika


- Presha kushuka


- Homa

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!