UGONJWA WA CHRONIC OSTEOMYELITIS

 chronic osteomyelitis

• • • • •

UGONJWA WA CHRONIC OSTEOMYELITIS


Osteomyelitis, haya ni maambukizi ya kwenye mfupa ambayo hutokea kwa njia mbali mbali kama vile;


 kupitia damu ambayo imebeba vimelea vya magonjwa, tisu ambazo zipo karibu na mfupa au mtu kupata ajali,jereha au kidonda ambacho kitafanya mfupa uonekane kwa nje hivo kuwa rahisi kwa wadudu(germs) kupenya na kuingia ndani ya mfupa.


CHANZO CHA UGONJWA WA OSTEOMYELITIS


- Kwa asilimia kubwa maambukizi haya hutokana na Bacteria jamii ya STAPHYLOCOCCUS ambao hupenya kwenye mfupa kwa njia mbali mbali kama vile;


✓ Kupitia jeraha au kidonda


✓ Kupitia kwenye damu


✓ Kwa mtu baada ya kufanyia upasuaji

n.k


DALILI ZA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;


- joto la mwili kupanda au mtu kuwa na homa


- Mtu kuchoka kupita kiasi


- Kupata maumivu makali kwenye mfupa ambao umeathiriwa


- Sehemu iliyoathiriwa kuvimba, kuwa na joto zaidi, kubadilika rangi na kuwa nyekundu n.k


WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO HILI


• Wavutaji wa sigara


• Watu ambao wana magonjwa kama kisukari, figo kufeli n.k


• Watu wenye kinga ndogo ya mwili


• Watu waliofanyiwa upasuaji


• Watu wenye magonjwa yoyote yanayohusu mfumo wa damu kama Sickle cell anemia n.k


• Wagonjwa wanaopata huduma mbali mbali hospitalini kama vile; kupata dawa kwa njia ya mshipa yaani Intravenous injection(IV), wanaowekewa catheter,wanaopata huduma ya dialysis n.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


Tiba kuu ya tatizo la Osteomyelitis ni, mgonjwa kufanyiwa upasuaji na sehemu ya mfupa iliyoathiriwa kuondolewa,


japo kuna njia nyingine za matibabu kama vile matumizi ya antibiotics kuuwa hawa bacteria N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!