UGONJWA WA DYSTONIA(chanzo,dalili na tiba)

  DYSTONIA

• • • • •

UGONJWA WA DYSTONIA(chanzo,dalili na tiba)


Dystonia ni ugonjwa ambao huhusisha misuli ya mwili kusinyaa bila mtu kupanga yaani Involuntary contract, hali ambayo huathiri misuli ya mwili,mjongeo wake n.k


Tatizo hili huweza kuathiri misuli ya eneo flani la mwili au ukaathiri mwili mzima.


CHANZO CHA TATIZO HILI


- Hakuna sababu ya moja kwa moja ya mtu kupatwa na tatizo hili japo zipo baadhi ya sababu ambazo huongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili kama vile;


• Mtu kurithi baadhi ya vinasaba vya tatizo hili katika familia au koo flani


• Matatizo katika mawasiliano ndani ya mfumo wa fahamu kwenye ubongo yaani nerves-cell communication problems

n.k


DALILI ZA TATIZO HILI


- Dalili za ugonjwa huu hutegemea na eneo ambalo limeathirika,


✓ Kama ni shingoni, Shingo ya mtu hupinga upande mmoja bila kunyooka hata akitembea


✓ Macho ya mgonjwa kucheza cheza na wakati mwingine macho kufunga yenyewe bila yeye kupanga, hivo kusababisha mtu huyu asione


✓ Viungo mbali mbali vya mwili kupinda kama vile; mikono,miguu na vidole vyake


✓ Mtu kushindwa kufanya shuhuli yoyote kama kuandika n.k


✓ Mtu kushindwa kuongea, kumeza kitu kooni n.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


- Tatizo hili halina tiba, japo kuna huduma mbali mbali huweza kufanyika kwa mgonjwa wa tatizo hili kama vile; dawa za kupunguza na kudhibiti dalili zake, au upasuaji wa kurekebisha mfumo wa nerves, ubongo n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!