Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA IDI ( EMERGING INFECTIOUS DISEASES,EID)



IDI

• • • • • •

UGONJWA WA IDI ( EMERGING INFECTIOUS DISEASES,EID)


Haya ni makundi ya magonjwa ya binadamu ambayo tunayaona yakimpata binadamu kwa mara ya kwanza. Dunia imekua ikipitia kipindi kigumu cha kukumbana na magonjwa haya kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita. Magonjwa haya aidha yalikuwepo na yalikua hayajulikani na yanaanza kuonekana au ni magonjwa mapya kabisa.


 Kwa magonjwa yalokuwepo lakini yanaanza kuonekana kwa binadamu sababu kubwa imekua ni mabadiliko ya vimelea wenyewe,kusambaa kati ya eneo na eneo na kuongezeka kwa kasi ya usugu wa vimelea(they may be new infections resulting from changes or evolution of existing organisms, known infections spreading to new geographic areas or populations, previously unrecognized infections appearing in areas undergoing ecologic transformation, or old infections reemerging because of antimicrobial resistance in known agents or breakdowns in public health measures).



Ugonjwa wa IDI umekua ukiongezeka na takribani asilimia 15 ya watu wanakumbana na hali hii. Ugonjwa wa IDI unaweza kuambikizwa kwa njia ya hewa,maji,vyakula visivyo salama,ngono zembe nk (EID may be foodborne, vector-borne, or airborne.)


Mfano wa magonjwa haya ni;


1)Candida auris


2) Elizabethkingia anopheles


3) SARS COV-2 (COVID-19)


4) Ebola Hemorrhagic Fever (Ebola virus disease)


5) Middle East Respiratory Syndrome (MERS)


6) Chikungunya Virus


7) H1N1 Influenza Virus (Swine Flu) 


8) Avian Influenza (Bird Flu)


9) zika


10) Hantavirus


Rejea ya atiko hii: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7096727/







Post a Comment

0 Comments