Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA MTU KUJIDHURU MWENYEWE(self-injury behavior)



 AFYA YA MWILI

• • • • • •

UGONJWA WA MTU KUJIDHURU MWENYEWE(self-injury behavior)


Hili ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, ambapo mtu huwa na tabia ya kujiumiza mwenyewe,kujidhuru kwa kujichoma na vitu vyenye ncha kali kama kisu,chupa,sindano, Kujiunguza kwa moto N.k


Pale ambapo anapopandisha hasira, kuumizwa kihisia, kuhisi kuonewa, N.k



CHANZO CHA TATIZO HILI


- Sababu kubwa za tatizo hili ni;


• Mtu kupoteza uwezo wa kuendana na mazingira aliyopo yaani Difficulty copiny skills


• Pamoja na Mtu kutokuwa na uwezo wa kutosha wa kudhibiti kiwango cha hisia mwilini yaani Difficulty managing emotions, baada ya kufanyiwa vitu mbali mbali kama vile; kukasirishwa, kukataliwa, kuhisi hali ya upweke, kuhisi kuonewa, n.k


Hivo Mtu huyu huona hali ya unafuu baada ya kufanya mambo mbali mbali kwenye mwili wake kama vile;


✓ Kujiunguza kwa moto


✓ Kujichoma kwa vitu vya ncha kali


✓ au kujiumiza kwa namna nyingine yoyote ile


DALILI ZA MTU MWENYE TATIZO HILI LA KUJIDHURU MWENYEWE


- Mtu kuwa na makovu mbali mbali kwenye mwili wake


- Mtu kuwa na vidonda mbali mbali mwilini ambavyo bado havijapona


- Mtu kuwa na malenge lenge ya kuungua kwa moto


- Mtu kuwa na historia ya kuumia mara kwa mara


- Mtu kupenda kutembea na vitu kama kisu


- Mtu kuongea maneno yanayoashiria upweke,kujiona sio wathamani duniani, kuhisi kukataliwa na kila mtu N.k


WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATWA NA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


1. Walevi


2. Wanaotumia madawa ya kulevyia,wavutaji bangi N.k


3. Watu wenye matatizo ya akili


4. Wanaokutana na mambo magumu ya kukatisha tamaa kila mara


5. Wenye marafiki wenye tatizo hili

N.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


Tiba ya tatizo hili hutegemea sana na chanzo chake, hivo mtu mwenye tatizo hili ataongea na wataalam wa afya na kuhojiwa kwa kina pamoja na kufanyiwa vipimo mbali mbali vya akili n.k, 


Ndipo tiba mbali mbali zianze,kama vile; matumizi ya dawa za magonjwa ya akili, huduma ya kisaikolojia yaani Psychotherapy N.k



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments