Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA NGOZI UNAOJULIKANA KAMA NEURODERMATITIS



 neurodermatitis

• • • • •

UGONJWA WA NGOZI UNAOJULIKANA KAMA NEURODERMATITIS


Neurodermatitis, ni ugonjwa wa ngozi ambao huhusisha ngozi ya mwili kuwasha sana, ngozi kuwa na wekunduwekundu pamoja na gamba la ngozi kutoka kwa baadhi ya wagonjwa,


Ugonjwa huu wa ngozi hupenda sana kushambulia maeneo ya shingoni, matakoni,mikononi na miguuni


CHANZO CHA UGONJWA HUU


- Mpaka sasa Hakuna sababu ya moja kwa moja ya kutokea ugonjwa huu, ila kuna kundi la watu ambalo limeonekana kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa huu wa neurodermatitis, kundi hilo ni kama vile;


1. Wanawake zaidi ya wanaume


2. Watu ambao wana umri wa kati ya miaka 30 na 50


3. Watu ambao washawahi kupatwa na tatizo hili hapo kabla wapo kwenye hatari ya kupata tena


4. Watu ambao wana matatizo mengine ya ngozi kama vile; eczema, psoriasis n.k


5. Watu wenye tatizo la hofu na wasiwasi kupita kiasi yaani Anxiety disorder


6. Watu wenye matatizo ya mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune diseases

n.k


DALILI ZA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;


- ngozi ya mwili kuwasha sana


- Kupatwa na madoa doa mekundu sehemu ya miwasho kwenye ngozi


- Ngozi kunyonyoka kwa baadhi ya watu


KUMBUKA, tatizo hili likiwa endelevu huweza kusababisha madhara mbali mbali kama vile;


✓ Ngozi kubadilika rangi kabsa


✓ Kupatwa na miwasho endelevu


✓ Mtu kuwa na makovu ya kudumu kwenye ngozi


MATIBABU YA UGONJWA HUU


- matibabu ya tatizo hili huhusisha njia mbali mbali kama vile; matumizi ya dawa za kupaka jamii ya corticosteroid cream , Dawa za tatizo la wasiwasi(Anxiety disorder),  na huduma zingine kama vile; Psychotherapy n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments