Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA NGOZI WA SEBOREIC DERMATITIS



MAGONJWA YA NGOZI

• • • • • •

UGONJWA WA NGOZI WA SEBOREIC DERMATITIS


Huu ugonjwa unaitwa seboreic dermatitis,ni ugonjwa wa Ngozi ambao unakua na tabia ya kuja na kuondoka ambao hupelekea Ngozi kujaa mafuta kama picha inavoonyesha. 


Ni ugonjwa ambao huwapata sana sana Watoto wadogo na watu wazima. Watu wenye VVU/UKIMWI hupata sana ugonjwa huu au unakua na makali Zaidi. Kisababishi cha ugojwa huu mpaka navoandika Makala hii hakijulikani. Kuna tetesi kidogo na tafiti zinaendelea kwamba kimelea Mallasezia anawez akahusika hapa.


Matibabu ya ugojwa huu yapo,yanategemea na kama una ugonjwa huo au una magonjwa mengine kama UKIMWI nk. Baada ya kujua kama kuna shida nyingine au la basi unaweza kupata dawa za kupaka kama ketoconazole, ciclopirox, olamine, tacrolimus, pimecrolimus, hydrocortisone, betamethasone, Zinc pyrithione, lithium sulfate, Selenium sulfide, salicylic acid na coal tar. Kadhalika kutokana na hali ya ugonjwa wako daktarin anaweza kukupa dawa za sindano au vidonge kama itraconazole, ketoconazole, fluconazole, terbinafine. Cc: Dr. mathew


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments