SINASI
• • • • • •
UGONJWA WA SINASI (RHINOSINUSITIS)
Huu ni ugonjwa wa kuvimba(infamation) ndani ya pua(nasal mucosa) na njia za wazi za karibu na pua(sinuses) usababishwao na virusi na bakteria
Kabla hatujaendelea inatupasa kuelewa muundo wa pua na maeneo yake Jirani Pamoja na hizo njia za wazi(sinus) na mpangilio wake.
Pua kwa ndani ina Ngozi laini Pamoja na mipangilio ya vichujio wa hewa(turbinates), vile vile ndani ya pua kumeungaishwa na njia za wazi za maksila(maxillary sinus),esimoidi(ethmoid sinus),njia za wazi za mbele(frontal sinus) na sfeno(sphenoid sinus) . Angalieni picha hapo juu kw uelewa wa zilivokaa
VISABABABISHI VYA UGONJWA WA SINASI
1) VIRUSI; virusi ndio visababishi vikuu vya ugonjwa was sinasi,karibia asilimia 95 ya wagonjwa wa sinasi kisababishi hu ani virusi. Virusi wanaohusika kulete ugonjwa wa sinasi kwa kiasi kikubwa ni rhinovirus, influenza virus, na parainfluenza virus
2) BAKTERIA; asilimia chache ya wagonjwa wa sinasi kisababishi hu ani bakteria na mara zote hu ani baada ya kupata sinasi ya virusi na ndipo bakteria huingia hapo. Bakteria wanaohusika na kulete sinasi ni Streptococcus pneumoniae, Haemophilus influenzae na Moraxella catarrhalis
MAKUNDI YA UGONJWA WA SINASI
1) Sinasi ambayo dalili zake hazidumu Zaidi ya wiki 4(Acute rhinosinusitis)
2) Sinasi ambayo dalili zake hukaa Zaidi ya wiki nne lakini hazidumu Zaidi ya wiki 12(Subacute rhinosinusitis)
3) Sinasi ambayo dalili zake hukaa Zaidi ya wiki 12(Chronic rhinosinusitis)
4) Sinasi inayjirudia rudiam(Recurrent acute rhinosinusitis)-mgonjwa anakua na historia ya kuumwa sinasi Zaidi ya mara nne kwa mwaka
WALIO KWENYE HATARI YA KUUGUA SINASI
1. Wazee
2. Wanaoogelea
3. Watu wenye maambukizi ya H-Pylori
4. Wenye mzio wa aina yeyote
5. Wanaovuta sigara na moshi wa sigara
6. Wanaosafiri safari mara kwa mara
7. Wanaosafiri kwa anga
8. Wenye pumu
9. Wenye magonjwa ya meno na kinywa
10. Wenye upungufu wa kinga mwilini. Cr:Dr.mathew
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!