Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA UVIMBE KWENYE KIFUNDO,AU KUOTA NYAMA KWENYE KIGANJA CHA MKONO(ganglion cyst)



KIGANJA
• • • • •
UGONJWA WA UVIMBE KWENYE KIFUNDO,AU KUOTA NYAMA KWENYE KIGANJA CHA MKONO(ganglion cyst)


Tatizo la Ganglion cyst ni tatizo ambalo huhusisha mtu kuwa na uvimbe kwenye kifundo(joint) au nyama kwenye eneo la nyuma kidogo ya kiganja cha mkono.


CHANZO CHA TATIZO LA GANGLION CYST


- Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ya kusababisha tatizo hili, japo kuna makundi ambayo yapo kwenye hatari zaidi kupata ugonjwa huu kama vile;


• Wanawake hupata zaidi ya wanaume


• Watu wenye matatizo ya mifupa kama vile shida ya osteoarthritis


• Watu wenye umri wa kati ya miaka 20 mpaka 40


• Mtu kuumia kwenye joints au vifundo hivo vya kiganjani na maeneo mengine


DALILI ZA UGONJWA WA GANGLION CYST


- Mtu kupata maumivu makali kwenye joint au kifundo cha mkono


- Kupata uvimbe kwenye joint au kifundo cha mkono,uvimbe huu huwa nyuma kidogo kwenye kiganja cha mkono, japo pia tatizo hili huweza kuathiri maeneo mengine kama vile kwenye magoti


- Mtu kushindwa kusogeza au kuzungusha kiganja cha mkono


MATIBABU YA UGONJWA WA GANGLION CYST

- Kama mgonjwa hapati maumivu yoyote, hali ya kushindwa kuzungusha kiganja n.k mgonjwa atashauriwa kuendelea kusubiri kwani tatizo huisha,


Ingawa kama anapata maumivu makali, kushindwa hata kusogeza mkono n.k basi njia mbali mbali za kimatibabu kama vile; Dawa pamoja na upasuaji huweza kutumika.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments