MJAMZITO
• • • • • •
CHANZO CHA MJAMZITO KUCHUKIA HARUFU YA MUME WAKE
Mama mjamzito huweza kumchukia mume wake kupita kawaida hasa pale anaposikia harufu yake tu,
Wanaume wengi hawajui kwamba mwanamke mjamzito huweza kupatwa na hali hii bila yeye kupanga,kitu ambacho huweza kumsababisha mwanaume kuwa na mawazo sana.
Kama wewe ni mwanaume unapitia hali kama hii,wala sio kwamba mke wako hakupendi tena, ni mabadiliko tu ambayo yamempata ambayo yapo Nje ya uwezo wake,
Je hali hii husababishwa na nini?
CHANZO CHA MJAMZITO KUCHUKIA HARUFU YA MUME WAKE
- Mwanamke mjamzito kuchukia harufu ya mume wake,hutokana na mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini kipindi cha ujauzito,ambayo huathiri mpaka mfumo unaohusika na kunusa au harufu yaani Smell sense center.
Hali hii hupelekea mama mjamzito kuhisi harufu mbaya hata kwa vitu ambavyo kwa hali ya kawaida havina harufu mbaya.
KWA UFUPI TU MABADILIKO YA VICHOCHEO MWILINI KIPINDI CHA UJAUZITO HULETA MABADILIKO MENGI MWILINI KAMA VILE;
- mwanamke mjamzito kutema sana mate mara kwa mara
- mwanamke mjamzito kuhisi kichefuchefu na kutapika
- Kupatwa na kiungulia cha mara kwa mara au Heartburn
- Mabadiliko ya ngozi ya mwili
- Matiti kujaa kuliko kawaida
- mama mjamzito kukosa usingizi kabsa
- mama mjamzito kuchukia harufu za vitu mbali mbali kama vile; baadhi ya perfumes,mafuta,n.k
- mama mjamzito kuchukia sana baadhi ya vyakula
- ladha ya mdomoni kubadilika kabsa
- mama mjamzito kuanza kupenda harufu za vitu ambayo kwa hali ya kawaida huwezi kuvipenda,mfano; harufu ya mkojo, viatu n.k
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!