TUMBO
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA TUMBO KUZALISHA KIWANGO KIKUBWA CHA ACID
Tatizo la uzalishaji wa kiwango kikubwa cha acid tumboni au gastric Acid ni tatizo ambalo huweza kumpata mtu yoyote na kuleta madhara makubwa sana mwilini.
CHANZO CHA UZALISHAJI WA KIWANGO KIKUBWA CHA ACID TUMBONI
Chanzo kikubwa ni kuzalishwa kwa kiwango kikubwa cha hormone ambayo hujulikana kama GASTRIN,
Hormone hii ndyo inatoa taarifa kuhusu kiwango cha uzalishaji wa acid tumboni yaani Gastric acid.
Uzalishwaji wa kichocheo hiki cha GASTRIN kupita kiasi huchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;
- Maambukizi ya Bacteria kama HELICOBACTER PYLORI
- Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo hupunguza kiwango cha acid tumboni
- Tatizo la Zollinger-Ellison syndrome
- Tatizo sugu la Figo kufeli yaani Chronic Kidney failure
- Njia ya kutoka tumboni kwenda kwenye utumbo mdogo kuziba
N.k
DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
✓ maumivu makali ya tumbo hasa ukiwa na Njaa
✓ tumbo kujaa gesi mara kwa mara
✓ kuhisi kichefuchefu na kutapika
✓ Uzito wa mwili kushuka kwa kasi sana
✓ Hamu ya chakula kupotea kabsa
✓ Kupata tatizo la kiungulia au Heartburn mara kwa mara
MADHARA YAKE
tatizo hili huweza kusababisha madhara mbali mbali kama vile;
- Mtu kuwa na vidonda vya tumbo
- Tatizo la kuvuja damu ndani ya tumbo
N.k
MATIBABU YA TATIZO HILI
Tatizo hili hutibika kwa kutumia dawa mbali mbali kama vile; Omeprazole, na aina nyingine za antibiotics, pia mgonjwa hupewa dawa mbali mbali za kudhibiti dalili kama vile; Kichefuchefu,kutapika,kiungulia,n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!