FAHAMU KWA KINA KUHUSU KIPIMO CHA KUPIMA MIMBA UPT yaani Urinary pregnancy test

  UPT

• • • • •

FAHAMU KWA KINA KUHUSU KIPIMO CHA KUPIMA MIMBA UPT yaani Urinary pregnancy test


UPT ni kipimo cha kupima mimba kwa Njia ya mkojo ambapo kirefu chake ni urinary pregnancy test,


Wanawake wengi hutumia kipimo hiki ili kuangalia kwamba wana Mimba au la!


JE KIPIMO HIKI CHA UPT KINAFANYAJE KAZI?


Ufanyaji kazi wa kipimo cha UPT kwenye mkojo hutegemea na Kichocheo au hormone inayojulikana kwa jina la human chorionic gonadotropin(HCG),


Hapa ndipo tunaweza kupata majibu ya aina mbili yaani;


1. Postive/reactive- mwanamke ni mjamzito


2. Negative/non-reactive- au mwanamke sio mjamzito


HUMAN CHORIONIC GONADOTROPIN HORMONE(HCG)


- Hii ni hormone ambayo huzalishwa na Placenta au kondo la nyumba,ndipo baadae huwepo ndani ya Mkojo, 


Na wataalam wanasema hormone hii huzalishwa kutoka kwa Placenta kuanzia siku ya 10,12 N.k Baada ya urutubishaji wa yai.


KUPIMA MIMBA KWA KUTUMIA UPT


- Mwanamke atatumia kipimo cha UPT ambapo ataweka kipimo chake kwenye Mkojo ili kisome,


Na majibu yatakuwa hivi;


1. Endapo mwanamke ni mjamzito na kichocheo cha HCG kimezalishwa na Placenta na kuwepo ndani ya Mkojo, basi majibu yataonyesha MISTARI MIWILI KWENYE KIPIMO au Mistari zaidi ya Mmoja.


2. Na endapo mwanamke sio mjamzito, basi hakuna kichocheo chochote cha HCG ambacho kinaweza kuwepo kwenye mkojo,hivo kipimo kitasoma MSTARI MMOJA TU wa Control.


Ni matumaini yangu kwamba umepata mwanga kuhusu kipimo hiki cha UPT.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!