JINSI YA KUZUIA MIMBA KWA KUTUMIA KALENDA

 MIMBA

• • • • •

JINSI YA KUZUIA MIMBA KWA KUTUMIA KALENDA


Kalenda ni mojawapo ya Njia ya Uzazi wa mpango ambayo ni salama zaidi kwani haisababishi mabadiliko yoyote mwilini ikiwemo badiliko la Vichocheo vya mwili


Japo njia hii ni ngumu sana kutumia Kwa mwanamke ambaye ana aina ya Mzunguko wa HEDHI ambao unabadilika badilika yaani IRREGULAR MENSTRUAL CYCLE


VITU VYA KUZINGATIA WAKATI UNATUMIA KALENDA KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO


- Hakikisha mzunguko wako wa Hedhi sio wa kubadilika badilika uwe STABLE/REGULAR MENSTRUAL CYCLE, namaanisha,kama mzunguko wako unachukua siku 28, iwe siku 28 mizunguko yote, Sio leo ni 28, kesho 21, kesho kutwa 35.


Mwanamke mwenye mzunguko wa hedhi ambao unabadilika badilika, njia hii sio nzuri kwake,kwani yupo kwenye hatari ya kubeba mimba bila kutarajia


- Ujue vizuri mzunguko wako wa Hedhi kabla ya Kuchagua njia hii ya Kalenda Kama Njia ya kuzuia Mimba


- Pata Elimu ya kutosha kutoka kwa Wataalam wa Afya juu ya Njia hii ya Kalenda kwenye Kuzuia mimba


- Hakikisha unaweka kumbukumbu zako vizuri kuhusu tarehe na kila mzunguko wako unavyokwenda kila mwezi


FAIDA ZA KUTUMIA KALENDA KUZUIA MIMBA


✓ Ni njia ambayo ni salama kwa asilimia 100%


✓ Ni njia ambayo haiwezi kusababisha mabadiliko yoyote ya vichocheo mwilini


✓ Ni njia ambayo haiwezi kuleta matatizo mbali mbali kwenye mzunguko wako wa hedhi mfano; Kublid bila mpangilio, Kublid damu nyingi na kwa muda mrefu, kukaa kwa muda mrefu bila kuona period,kublid vitone vitone tu n.k


✓ Ni njia ambayo haina maudhi madogo madogo kama vile; Maumivu makali ya kichwa mara kwa mara,kichefuchefu n.k


MADHARA YA KUTUMIA KALENDA KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO


• Ni rahisi sana Mwanamke kupata mimba kama hajui vizuri mzunguko wake wa Hedhi


• Njia hii haifai kwa mwanamke mwenye mzunguko wa Hedhi ambao hubadilika badilika


• Huhitaji Umakini mkubwa sana kuliko Njia nyingine za kuzuia mimba


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!