KUWASHWA MATAKONI (PRURITUS ANI)

 MIWASHO

• • • • • •

KUWASHWA MATAKONI (PRURITUS ANI)


Hii ni hali ambayo mtu anakua anawashwa maeneo ya puru na maeneo jirani. Ni ugonjwa ambao huwapata watu wengi sana na  kwa kweli imekua ni hali inayokera .hali hii inapokua inakera basi ndo tunashauri itibiwe.Hali hii inawapata watu sana na takribani asilimia 5 ya watu wanapata hali hii na wanaume ndo wanapatwa sana kuliko wanawake


VISABABISHI VYA HALI HII


Kwa wakati mwingine kisababishi cha hali hii kinaweza kisijulikane; baadhi ya visababishi ni kama ifuatavyo


1)MINYOO


2)UTITIRI


3)STRESS


4)BAWASIRI


5)KISUKARI,MAGONJWA YA DUNDUMIO NK


6)PUMU YA NGOZI


7)MAGONJWA YA ZINAA(kwa wanaofanya mapenzi ya njia ya haja kubwa)


8)SABUNI NA KEMIKALI(hii ni kwa wale wanaotumia sabuni zenye madawa au wipers kwa ajili ya kujisafisha maeneo ya haja kubwa)


9)UGONJWA WA SORIASISI


10)FANGASI


11)UCHAFU(kuvaa nguo za ndani chafu,kuacha chembechembe za kinyesi  baada ya kujisaidia nk)


MATIBABU NA KUJITUNZA


Hali hii inatibika vizuri kabisa na hasa kama kisababishi kikijulikana. Ugonjwa huu unatibiwa kwa dawa za kumeza,kupaka na hata sindano kulingana na kisababishi. Kujilinda na hali hii usioshe kwa sabuni maeneo ya haja kubwa,kula mboga za majani mara kwa mara,usive chupi au boksa zinazobana,weka maeneo ya haja kubwa na jirani kukavu muda wote na USIJIKUNE maeneo ya haja kubwa. Cr:Dr.mathew




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!