Mabadiliko ambayo mwanaume huyapata Baada ya mke wake kuwa Mjamzito(HERI YA SIKU YA AKINA BABA DUNIANI)
happy father's day
• • • • • •
Mabadiliko ambayo mwanaume huyapata Baada ya mke wake kuwa Mjamzito(HERI YA SIKU YA AKINA BABA DUNIANI)
Japo akina baba wengi huonekana kutojihusisha sana na ujauzito, ukweli ni kuwa wanajali japo wengi wao hawaoneshi dhahiri. Mama humbeba mtoto tumboni ila BABA HUMBEBA MTOTO KICHWANI NDANI YA MAWAZO YAKE.
Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Michigan ulioongozwa na Prof. Robin Edelstein unaeleza kuwa baadhi ya wanaume hupitia mabadiliko ya homoni (hormonal changes) kipindi wenza wao wanapokuwa wajawazito, kwa homoni ya kiume ya Testosterone kushuka kama vile inavyokuwa kwa wenza wao.
Prof huyo anaeleza kuwa hakuna ushahidi kwa nini wanaume pia hupungua homoni hiyo kama wenza wao lakini anahusisha na wazo kuwa:
Wanaume hao ni wale wenye kuwajali zaidi wenza wao (better caregivers) kwa kuwa hupunguza ukali (aggressiveness) unaohusishwa na kiwango cha juu cha homo hiyo.
HERI YA SIKU YA AKINA BABA DUNIANI!!!
Cr:afyabongo
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!