Ticker

6/recent/ticker-posts

MADHARA YA KULA MAYAI AMBAYO HAYAJAIVA VIZURI AU MABICHI



  MAYAI

• • • • • •

MADHARA YA KULA MAYAI AMBAYO HAYAJAIVA VIZURI AU MABICHI


Baadhi ya watu hupenda kula mayai ambayo ni mabichi kwa sababu mbali mbali kama vile; kwa dhana ya kurekebisha sauti kwa waimbaji, kuponya kikohozi n.k


Lakini pia kuna wengine hupenda kula chips yai ambayo haijakaushwa vizuri,


 Je kula mayai mabichi au ambayo hayajaiva vizuri kuna madhara?


Baadhi ya tafiti za Wataalam wa afya zinaonyesha kwamba mayai mabichi au ambayo hayajaiva vizuri huweza kuwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Bacteria jamii ya Salmonella Enteritidis PT4,


ambao huweza kumshambulia mtu na kusababisha matatizo mbali mbali kama vile;


✓ joto la mwili kuwa juu sana au mtu kuwa na homa kali


✓ Tatizo la maumivu makali ya tumbo


✓ Tatizo la kuharisha


✓ Mwili kukosa nguvu na kuchoka kupita kiasi


✓ Kuhisi kichefuchefu na kutapika mara kwa mara


✓ Au mtu kuwa na tatizo la Homa ya matumbo


Kula mayai mabichi kwa kipindi kirefu huweza kusababisha madhara mengine kama vile;


• tatizo la Ulimi kupasuka wenyewe kutokana na upungufu mkubwa wa Vitamin B


• Pia baadhi ya tafiti huonyesha kwamba,ute mweupe wa Yai huweza kusababisha upungufu wa BIOTIN kwenye mwili wako

N.k


kutokana na Sababu hizo,ulaji wa mayai mabichi au ambayo hayajaiva Vizuri sio salama kwa Afya yako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments