MATATIZO YA MTOTO YANAYOTOKANA NA MAMA KUNYWA POMBE wakati wa Ujauzito(Fetal Alcohol Syndrome)

   FETAL ALCOHOL SYNDROME

• • • • •

MATATIZO YA MTOTO YANAYOTOKANA NA MAMA KUNYWA POMBE wakati wa Ujauzito(Fetal Alcohol Syndrome)


Matatizo ambayo huweza kumpata mtoto baada ya mama kunywa pombe wakati wa ujauzito hujulikana kwa kitaalam kama Fetal alcohol syndrome,


Madhara ya mama mjamzito kunywa pombe sio kwa mtoto tu aliyetumboni hata kwa mama mwenyewe, ila katika makala hii tunachambua kwa kina madhara kwa mtoto baada ya mama kunywa pombe wakati wa ujauzito


MATATIZO YA MTOTO YANAYOTOKANA NA MAMA KUNYWA POMBE wakati wa Ujauzito(Fetal Alcohol Syndrome)


- Tatizo la kuharibika kwa ubongo yaani brain damage


- Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo sana


- Mtoto kudumaa au kuchelewa kwenye kila hatua ya ukuaji


- Mtoto kuwa na macho madogo sana kuliko kawaida


- Lips za juu kwenye mdomo kuwa nyembamba


- Kuwa na pua fupi na ambayo imegeukia juu


- Kuwa na matatizo ya joints


- Kuwa na matatizo ya macho ikiwa ni pamoja na shida ya macho kuona


- Kuwa na matatizo ya kutokusikia vizuri


- Mtoto kuzaliwa na kichwa kidogo sana


- Kuwa na matatizo ya figo


- Kuwa na matatizo ya moyo


- Ngozi ambayo huunganisha pua na lips za juu ya mdomo kuwa nyembamba na laini sana


- Kuwa na tatizo la kusahau vitu haraka au kupoteza kumbukumbu


- Kubadilika mood kwa haraka zaidi


- Kuwa mtu wa kufanya maamuzi ya haraka na ambayo sio sahihi

n.k


CHANZO CHA TATIZO


• Baada ya mama mjamzito kunywa pombe, Pombe huingia moja kwa moja kwenye mzunguko wa damu na kupita kwenda kwa mtoto kupitia kwenye kondo la nyuma au placenta, kisha huanza kuleta madhara mbali mbali kwa mtoto kama nilivyokwisha kuelezea hapo juu,


Baada ya pombe kuingia kwenye damu  ambayo huenda moja kwa moja kwa mtoto huathiri usafirishaji wa hewa safi ya OXYGEN kwenda kwa mtoto pamoja na usafirishaji wa virutubisho muhimu kwa mtoto yaani nutrients,


Pombe huanza kuharibu tissu pamoja na viungo mbali mbali vya mtoto ikiwa ni pamoja na kuharibu kabsa Ubongo wake



KUMBUKA; Tatizo la Fetal Alcohol syndrome halina tiba, hivo ni muhimu sana mama mjamzito kuepuka matumizi ya pombe


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!