MAZIKO YA KISAYANSI-CAPSULA MUNDI-MWILI WAKO KUGEUKA MTI BAADA YA KUFA

FAHAMU

• • • • •

MAZIKO YA KISAYANSI-CAPSULA MUNDI-MWILI WAKO KUGEUKA MTI BAADA YA KUFA



U hali gani mdau wangu,leo nataka nishee na  wewe jambo moja na la muhimu sana kwa ulimwengu wetu na jambo lenyewe ni kuhusu kuzikwa bila jeneza na kugeuka mti baada ya kufa


Kama sote tujuavyo binadamu hufariki kila siku,huzikwa na wengine huzaliwa. Kumekua na taratibu za kuzika mwili ardhini kwa kutumia majeneza nk,kwa ndugu zetu wahindi wamekua wakichoma mwiliKuzika mwili kwenye majeneza kumekua hakuleti faida kwa jamii iliyobaki na san asana imekua ikichukua nafasi za ardhi ambayo hutumika kama makaburi;


ambayo ingekua na faida nyingine kwa viumbe walio hai.Ikumbukwe kwamba binadamu anapokufa mwili wake unakua una virutubisho vingi sana na ambavyo tunapoufukia mwili chini tunakua tumepoteza au kupata hasara kubwa kwani tutakua hatujapata faida za kimazingira kutokana na huo mwili


Kwa sasa kuna teknolojia ya capsula mundi ambayo binadamu aliefariji huwekwa kwenye mfuko maalumu wenye umbo la yai na ndipo huchimbiwa ardhini k pamoja na kuweka mbegu ya mti.


 Mwili huo unapokua unaoza kwa msaada wa bacteria basi mti utakaokua unaota hapo basi hunawiri na kukua vizuri kwani ule mwili utakua ni mbolea tosha yenye virutubisho vyote.


kadhalika heshima ya aliezikwa na kua mti itaendelea kuwepo na ndugu wataendelea kutoa heshima zao sema kwa sasa watakua wanatembea mashambani na kuona mti uliotokana na mwili wa Fulani.


Hii teknolojia ni nzuri sana kwani kwanza husaidia kulinda mazingira yetu kwa kuongeza idadi ya miti yenye afya,kupunguza hewa ya ukaa duniani,kuongeza kiasi cha hewa safi ya oksijeni,kupunguza madhara ya athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi na hizi faida ni kwa sababu ya miti mingi itakayoota kutokana na miili ya waliokufa. Huu ndo utakua mwisho wa matumizi ya majeneza na mwanzo wa kuongezeka kwa miti ulimwenguni.


Ama kweli hili ni jambo jema sasa,hebu fikiria watu wote walozikwa kwa majeneza wangezikwa kwa teknolojia hii tungekua na miti mingapi yenye afya?,tungepunguza adhari za mabadiliko ya hali ya hewa,tungepunguza kwa kiasi kikubwa upungufu wa mvua na ongezeko la joto dunia. Cr:Dr.mathew 




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!