MBILIKIMO
• • • • • •
MBILIKIMO NI UGONJWA AU NI NINI?(soma hapa kujua)
Mbilikimo kwa hali ya kawaida ni watu wafupi sana kupita kawaida, Watu hawa wamekuwa maarufu sana katika maeneo mbali mbali kama vile KONGO(DRC) n.k kutokana na ufupi wao.
Mbilikimo wamegawanyika kwa aina mbili;
- Kuna mbilikimo kutokana na asili ya watu wa jamii flani katika maeneo mbali mbali duniani
- Na kuna mbilikimo kama ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Dwarfism.
JE UGONJWA WA DWARFISM AU MBILIKIMO NI NINI?
Hili ni tatizo ambalo husababisha mtu kuwa mfupi sana kupita kawaida kutokana na sababu mbali mbali kama vile za vinasaba au Genetics na matatizo mengine ya kiafya.
Watu wenye tatizo la dwarfism huwa wafupi sana kwa kiwango cha chini au sawa na Cm 147,122 n.k ukipima urefu wao.
CHANZO CHA TATIZO HILI LA DWARFISM
- Asilimia kubwa ya watu wenye tatizo la Dwarfism hutokana na shida ya achondroplasia
- Tatizo lingine ni Turner syndrome,ambapo mwanamke huzaliwa huku akiwa hana chromosome moja(X), hivo badala ya kuwa na chromosome mbili (XX) kama wanawake wengine, humiss chromosome moja ya X.
- Matatizo ya vichocheo mwilini hasa vichocheo vinavyohusika na ukuaji wa mtu kuwa pungufu yaani Growth hormone deficiency
N.k
MATIBABU YA TATIZO HILI
- Hakuna tiba ya kuongeza Urefu wa mtu bali kuna Matibabu juu ya dalili mbaya ambazo huweza kumpata mtu mwenye shida hii kama vile; Kushindwa kutembea,kuongea vizuri, maumivu ya viungo N.k
Tiba hiyo huweza kuhusisha kuongeza kiwango cha vichocheo mwilini yaani Hormonal therapy, matibabu ya Upasuaji N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!