Ticker

6/recent/ticker-posts

NJIA ZA KUPUNGUZA SUKARI MWILINI BILA KUTUMIA DAWA



 KISUKARI

• • • • •

NJIA ZA KUPUNGUZA SUKARI MWILINI BILA KUTUMIA DAWA


1. Fanya mazoezi ya mwili kila siku angalau dakika 30 au nusu saa


2. Dhibiti kiwango cha Glucose kinachoingia mwilini


3. Ongeza kiwango cha kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi yaani FIBERS kama vile; Mboga za majani pamoja na matunda kama vile Machungwa, maembe n.k


4. Kula vyakula vyenye kiwango cha kutosha cha CHROMIUM na MAGNESSIUM au kwa kitaalam tunasema Micronutrient


- Mfano wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha CHROMIUM ni kama vile;


• Nyama


• Mboga za majani


• Karanga


• matunda

n.k


- Mfano wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha MAGNESSIUM ni kama vile;


• mboga za majani jamii ya Dark Leafy Green vegetable


• Ndizi


• Maharage


• maparachichi

n.k


Upungufu mkubwa wa Magnessium na Chromium(Micronutrient) mwilini huweza kusababisha kiwango cha sukari kwenye damu kuwa juu


5. Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala,


Ukosefu wa usingizi pamoja na muda wa kutosha wa kulala huchangia kiwango cha sukari kuwa juu


6. Fanya vipimo vya sukari mara kwa mara


7. Hakikisha unadhibiti kiwango cha mawazo na kuepuka Msongo wa mawazo,


Tafiti zinaonyesha kwamba vichocheo au hormones ambazo huzalishwa mtu akiwa na msongo wa mawazo yaani GLUCAGON na CORTISOL husababisha kiwango cha Sukari kwenye Damu kuongezeka


8. Hakikisha unakula vyakula vyenye kiwango kidogo cha GLYCEMIC index kwani huongeza kiwango cha sukari kwenye damu,


Mfano wa vyakula hivo ni kama vile;


- yogurt


- maharage


- mboga za majani

n.k


9. Hakikisha unapunguza uzito wa mwili na kuepuka tatizo la kuwa na uzito mkubwa kupita kawaida


10. Kunywa kiwango cha kutosha cha maji kila siku angalau Lita 2.5 mpaka 3 kila siku



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments