DAWA ZA MINYOO
• • • • •
Tofauti kati ya Dawa za Minyoo za ALBENDAZOLE na MEBENDAZOLE
Katika makala hii tunachambua kuhusu tofauti iliyopo kwenye hizi aina mbili za dawa za minyoo;
1. ALBENDAZOLE
- Hii ni dawa ya minyoo ambayo hutibu vizuri maambukizi ya minyoo jamii ya TAPEWORMS, neurocysticercosis, giardiasis,trichuriasis n.k
- Maudhi madogo madogo yanayoweza kutokea kwa baadhi ya watu baada ya kutumia dawa hizi ni pamoja na; kuhisi kichefuchefu, maumivu ya tumbo na maumivu ya kichwa
- Dawa ya Minyoo aina ya ALBENDAZOLE hufanya kazi vizuri sana juu ya maambukizi ya Minyoo jamii ya Tapeworms au Flatworms, Nematodes, Giardiasis, Microsporidiosis,granulomatous,amoebic encephalitis,Arthropods n.k
- Dawa hizi sio salama kwa MAMA MJAMZITO hasa katika miezi mitatu ya mwanzoni ya ujauzito yaani FIRST TRIMESTER kwani huweza kusababisha madhara katika uumbaji wa mtoto yaani Teratogenic effects
2. MEBENDAZOLE
- Dawa hizi kufanya kazi vizuri sana dhidi ya minyoo jamii ya PARASITIC WORMS kama vile; HOOKWORMS, Ascariasis, Pinworm N.k
- Dawa hizi ni salama kwa MAMA MJAMZITO, hivo huweza kutumiwa na mama akiwa na mimba
- Maudhi madogo madogo ambayo huweza kuwapata baadhi ya watu baada ya kutumia dawa hizi ni pamoja na; Kupata maumivu ya tumbo
- Dawa hizi ni salama kwa watoto kuanzia miaka 2
- Dawa hizi sio salama sana kwa Watu wenye umri mkubwa au wazee pamoja na watoto kuanzia umri wa miezi 6 mpaka miaka 2
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!