Ugonjwa wa Bipolar maana yake,dalili,chanzo,madhara na Tiba yake

 BIPOLAR

• • • • • 

Ugonjwa wa Bipolar maana yake,dalili,chanzo,madhara na Tiba yake


Ugonjwa wa Bipolar ambapo hapo mwanzoni ulikuwa unajulikana kama MANIC DEPRESSION, huu ni ugonjwa ambao huhusisha hali ya kiakili kuathiriwa na kusababisha mtu kukosa mood kabsa pamoja na mfadhaiko mkubwa


DALILI ZA UGONJWA WA BIPOLAR NI PAMOJA NA;


1. kufanya vitu kwa haraka haraka bila uangalifu


2. Mtu kuwa na tatizo la Kukosa usingizi kabsa au kulala sana kupita kiasi


3. Mtu kuwa na shida ya kuongea sana yaani unusually talkative


4. Mtu kuwa na mawazo ya haraka haraka


5. Mtu kufanya maamuzi ambayo sio sahihi kila mara


6. Mtu kupoteza tumaini,kuwa na huzuni sana na kukosa ari ya kufanya kazi


7. Mtu kulia kila mara bila sababu ya msingi


8. Uzito wa mwili kushuka kwa kasi sana au mtu kuongezeka uzito kwa kasi sana kuliko kawaida


9. Hamu ya chakula kupotea kabsa au hamu ya chakula kuongezeka na mtu kula sana kuliko kawaida


10. Mwili kuchoka kupita kawaida


11. Mtu kujiona mwenye makosa au hatia kila mara kwa kila kitu anachokifanya


12. Mtu kuwaza kujiua mwenyewe au kudhuru wengine

N.k


CHANZO CHA UGONJWA WA BIPOLAR


- Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo huhusishwa na tatizo hili,japo kuna baadhi ya sababu ambazo zimeonekana kuongeza uwezekano wa ugonjwa huu,na sababu hizo ni kama vile;


✓ Kuwa na ndugu wa karibu mwenye tatizo hili


✓ Kuwa na shida ya msongo wa mawazo kila mara


✓ Matumizi ya madawa ya kulevyia kupita kiasi ikiwa ni pamoja na unywaji wa pombe kupita kawaida


MADHARA YA UGONJWA HUU


• mtu kupata madhara mbali mbali mwilini kutokana na matumizi ya dawa za kulevyia au pombe kupita kiasi kwa mgonjwa wa Bipolar


• mtu kujiua mwenyewe au kudhuru wengine


• kupoteza uwezo wa kufanya kazi

N.k


MATIBABU YA UGONJWA WA BIPOLAR


Ugonjwa huu hutibiwa na wataalam wa afya ya Akili yaani psychiatrist,


ambapo matibabu yake yatahusu njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa kama vile; Lithobid,Olanzapine N.k


Hivo kutana na wataalam wa afya ya Akili, Au;


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!