LIVER CIRRHOSIS
• • • • • •
UGONJWA WA INI MAARUFU KAMA LIVER CIRRHOSIS
Hii inaitwa liver cirrhosis. Ni ugonjwa wa ini ambao hupelekea ini kua na makovu makovu (fibrosis) na hivo kuharibu utendaji wake. Ugonjwa huu hutokea kama matokeo ya magonjwa mbalimbali ya Ini yampatayo mtu.
Ugonjwa huu mpaka kufikia hapa ni matokeo mabadiliko ya ndani ya Ini ya muda mrefu na kwa kweli ugonjwa huu huanza kujitokeza taratibu taratibu na yaweza kuchukua miezi kadhaa au miaka kadhaa mpaka mtu aje kupata dalili zake au ajue ana huu ugonjwa
VISABABISHI VIKUU VYA HALI HII NI
1) Matumizi ya pombe nyingi kwa muda mrefu
2) Maambukizi ya virusi wa homa ya ini hasa hasa aina B na C
3) Maabukizi sumu kuvu (unaweza kuipata kwa kula vitu vyenye uvundo kama karanga,mahindi nk)
4) Unene
5) Maambukizi ya VVU/UKIMWI
6) Saratani ilosambaa kwenye ini au ya ini
7) Kichocho cha ini
8) matumizi ya madawa kiholela
DALILI ZA TATIZO HILI
Dalili za awali za ugonjwa huu ni
1) Kupoteza hamu ya kula
2) Uchovuuchovu
3) Kupungua uzito kusikoeleweka
4) Maumivu ya tumbo hasa upande wa kulia chini ya mbavu
5) Kichefuchefu na kutapika
Dalili za ugonjwa ambao ushakua mkubwa na kuleta madhara ni
1) Kuwashwa mwili
2) Kuvimba tumbo
3) Kuvimba miguu
4) Kupata manjano
5) Damu kutokuganda haraka unapoumia
Cr:Dr. mathew
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!