PCOS
• • • • •
UGONJWA WA POLYCYSTIC OVARY SYNDROME(PCOS),chanzo chake,dalili na Tiba
Polycystic ovary syndrome ni tatizo ambalo huhusisha hitilafu kwenye vichocheo vya mwili hasa kwa wanawake ambao wapo kwenye Umri wa kuzaa au reproductive age.
DALILI ZA TATIZO LA POLYCYSTIC OVARY SYNDROME(PCOS) ni pamoja na;
✓ Mwanamke kuwa na mzunguko wa hedhi ambao haueleweki(irregular menstrual period),kupata blid kwa muda mrefu mfano zaidi ya wiki moja au kukaa kwa muda mrefu bila kuona period hata zaidi ya miezi 3 n.k
✓ Mwanamke kuwa na nywele nyingi mwilini,usoni n.k
✓ Mwanamke kuwa na ndevu
✓ Mwanamke kuwa na kipara
✓ Mwanamke kuwa na chunusi sana usoni ambazo haziishi
n.k
CHANZO CHA TATIZO LA POLYCYSTIC OVARY SYNDROME(PCOS)
- Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo huhusishwa na uwepo wa tatizo hili,ila kuna baadhi ya sababu ambazo huongeza uwezekano wa tatizo hili kama vile;
1. Mwanamke kuwa na kiwango kikubwa cha hormone ya kiume inayojulikana kama ANDROGEN
2. Mwanamke kuwa na kiwango kikubwa cha hormone ya INSULIN ambayo huongeza uzalishaji wa Androgen
3. Tatizo la uvimbe kwenye vifuko vya mayai yaani Ovaries ambalo husisimua na kuhamasisha Ovaries kuzalisha androgen
4. Pia kurithi vinasaba vya tatizo hili katika familia au koo husika kwa kitaalam tunasema Heredity factor
MADHARA YA TATIZO LA POLYCYSTIC OVARY SYNDROME(PCOS) KWA WANAWAKE
• Mwanamke kushindwa kubeba mimba
• Kupata kisukari cha mimba yaani Gestational Diabetes
• Kupata presha wakati wa ujauzito yaani Pregnancy induced Hypertension
• Kupata kansa kwenye kuta za mji wa mimba
• Mwanamke kupata tatizo la Mimba kutoka zenyewe
• Kuzaa mtoto kabla ya wakati yaani Premature birth
• Kupata tatizo la uvimbe wa Ini
• Matatizo kwenye mfumo wa uchakataji wa chakula na vinywaji ndani ya seli kuzalisha nishati yaani metabolic syndrome
• Tatizo la kuwa na kiwango kikubwa cha Lehemu au Cholestrol mwilini
• Kuwa na tatizo la kisukari hasa Type 2 Diabetes
• Kuwa na shida ya msongo wa mawazo, wasi wasi mkubwa n.k
• Kuwa na shida ya kuvuja damu kwenye mji wa mimba yaani abnormal Uterine bleeding
N.k
MATIBABU YA TATIZO LA POLYCYSTIC OVARY SYNDROME(PCOS)
- matibabu ya tatizo hili huhusisha kudhibiti dalili zake kama vile;
• Tatizo la kuwa na mzunguko wa hedhi usio eleweka ambapo dawa mbali mbali hutumika kama vile Combined Oral contraceptives(COC's) n.k
• Dawa za kumsaidia mwanamke mwenye tatizo la kutokubeba mimba,
N.k
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!