Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA SELI MUNDU AU SICKLE CELL pamoja na Madhara yake



 SICKLE CELL

• • • • • •

UGONJWA WA SELI MUNDU AU SICKLE CELL pamoja na Madhara yake


Ugonjwa wa seli Mundu au sickle cell kama inavyofahamika kwa wengi, ni ugonjwa ambao huathiri Haemoglobin, sehemu muhimu sana kwenye muundo na ufanisi wa seli nyekundu za damu(Red blood cells)


Sickle cell ni miongoni mwa magonjwa ambayo huathiri sana watoto wadogo na kuleta madhara mbali mbali mwilini,


Wakati mwingine mgonjwa wa sickle cell hupatwa na hali ya maumivu makali katika sehemu mbali mbali za mwili wake pamoja na tatizo la kuishiwa na Damu,ikiwa ni pamoja na matatizo mengine kama vile;


1. Matatizo ya kuziba kwa mishipa midogo ya damu (Vaso-occlusive crisis): Kutokana na umbile lake, kiini mundu au sickle cell huwa rahisi sana kuvunjika vunjika pindi zinapopita katika mishipa midogo midogo ya damu.


 Hali hii hupelekea kuziba kwa mishipa ya damu na hivyo kusababisha maumivu makali na kuzuia usambazaji wa oxijeni katika sehemu zilizozibwa, na hivyo kuathiri viungo vingine mwilini.


2. Matatizo ya damu kujilundika kwenye wengu (Splenic sequestration crisis): Katika hatua hii, wengu huathirika na huwa kubwa kuliko kawaida na pia huwa na maumivu makali.


 Hukusanya damu nyingi na kuvunja chembe nyekundu zote zilizoathirika na kusababisha upungufu wa ghafla wa damu mwilini.


3. Matatizo ya kupungua kwa damu (Aplastic crisis): Katika hatua hii, upungufu wa damu huzidi kuongezeka na kusababisha, mapigo ya moyo kwenda kwa kasi zaidi na hivyo kuvuruga kitendo cha kutengeneza chembe chembe nyekundu za damu au erythropoeisis kwa kuvamia na kuharibu vyanzo vyake.


4. Matatizo ya kuvunjwa vunjwa kwa chembe nyekundu za damu (Hemolytic crisis): Katika hatua hii, chembe chembe nyekundu za damu huvunjwa kwa wingi zaidi na kusababisha upungufu mkubwa wa damu.


5. Matatizo ya maumivu katika viganja (Dactylitis): Maumivu katika viganja vya mikono na miguuni hutokea mara nyingi kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi sita na zaidi.


6. Matatizo ya ghafla ya kifua (Acute chest syndrome): Katika ali hii, mgonjwa hupata homa, maumivu makali ya kifua, ushindwa kupumua vizuri, na iwapo mgonjwa atafanyiwa kipimo cha x-ray ya mapafu, kipimo kitaonesha mabadiliko yasiyo ya kawaida (pulmonary infiltrates). Cr: Drtareeq






Post a Comment

0 Comments