UPUNGUFU WA DAMU MWILINI KUTOKANA NA UPUNGUFU WA BAADHI YA VITAMINS(Vitamin deficiency anemia)
ANEMIA
• • • • • •
UPUNGUFU WA DAMU MWILINI KUTOKANA NA UPUNGUFU WA BAADHI YA VITAMINS(Vitamin deficiency anemia)
Tatizo la upungufu wa damu mwilini yaani ANEMIA huweza kusabibishwa na sababu mbali mbali kama vile; upungufu wa madini chuma, minyoo jamii ya hookworms,malaria,sicke cell anemia n.k
Ila katika makala hii tunachambua upungufu wa damu mwilini ambao hutokana na upungufu wa baadhi ya vitamins mwiliini ambapo kwa kitaalam hujulikana kama VITAMIN DEFICIENCY ANEMIA
Vitamin Deficiency anemia ni upungufu wa damu mwilini kutokana na upungufu wa vitamins muhimu na vitamins hizo ni kama vile; VITAMIN B9(folate), VITAMIN B12 Na VITAMIN C
CHANZO
- Ni mtu kutokula vyakula vyenye kiwango cha kutosha cha vitamins kama vile; Vitamin B9, Vitamin B12, na Vitamin C.
- Au mwili wenyewe kushindwa kufyoza na kuchakata hizi vitamins.
DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI KUTOKANA NA UPUNGUFU WA BAADHI YA VITAMINS(Vitamin deficiency anemia)
✓ Mapigo ya moyo kwenda mbio
✓ Mwili kuchoka kupita kiasi
✓ Mtu kushindwa kupumua
✓ Mwili kukosa nguvu kabsa na misuli ya mwili kuwa dhaifu
✓ Kubadilika rangi ya ngozi,mikono, lips za mdomo, kwenye macho n.k Na kuwa na weupe au Paleness
✓ Mtu kuwa na kizunguzungu
✓ Uzito wa mwili kupungua kwa kasi
✓ Dalili kama za mtu kuchanganyikiwa
N.k
KUMBUKA;
• Folate au Vitamin B9- hupatika kwa kiasi kikubwa kwenye matunda na mboga mboga za majani
• Vitamin B12- hupatikana kwa kiwango kikubwa kwenye nyama,mayai, maziwa n.k
• Vitamin C- hupatikana kwa kiwango kikubwa kwenye viazi,matunda kama machungwa n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!