Athari za Mafuta ya kula yaliyoharibika na jinsi ya kuepuka kutumia mafuta yaliyoharibika(Rancidity)

 RANCIDITY

• • • • • •

Athari za Mafuta ya kula yaliyoharibika na jinsi ya kuepuka kutumia mafuta yaliyoharibika(Rancidity)


Mafuta yaliyoharibika huweza kutambuliwa kwa harufu mbaya,kubadilika rangi n.k


Na hapa hatunzungumzii tu mafuta ya kununua dukani, bali hata mafuta kutoka kwa viumbe kama samaki walioharibika n.k


ATHARI ZA KULA MAFUTA YALIYOHARIBIKA


- Mafuta yaliyoharibika hufanya mchakato unaujulikana kama Oxidation kwenye seli hai za mwili wako ndipo madhara huanza kutokea japo sio pale pale bali huchukua muda kidogo,


Madhara hayo ni pamoja na;


✓ Kuharibiwa kwa seli hai za mwili


✓ Kuharibiwa kwa proteins,DNA N.k


✓ Lakini pia mchakato huu wa oxidation huongeza speed ya mtu kuzeeka haraka pamoja na kupatwa na magonjwa mbali mbali ya kudumu kama vile;



• Magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na mishipa ya moyo kuziba,moyo kuwa mkubwa,kuvimba n.k


• Tatizo la saratani au kansa mbali mbali


• Pamoja na matatizo ya uvimbe kwenye maeneo mbali mbali mwilini


JINSI YA KUEPUKA KUTUMIA MAFUTA YALIYOHARIBIKA


1. Utunzaji wa mfuta: weka mafuta kwenye sehemu ya ubaridi pamoja na kutumia vyombo visafi vya kuhifadhia mafuta


2. Epuka kununua mafuta mengi kwa wakati mmoja ambayo yatakaa kwa muda mrefu


3. Angalia Expire date wakati unanunua mafuta dukani


4. Epuka kula samaki walioharibika


5. Chagua mafuta ambayo hayagandi ni mazuri zaidi



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!