MAKEUP
• • • • •
Madhara ya Kutumia Makeup Kila siku(Kwa wanawake)
Kufanya makeup kila mara usoni kwa wanawake,imekuwa fashion kwa hivi sasa, je unafahamu kwamba kuna madhara mtu huweza kupata kwa kufanya makeup? soma hapa
MADHARA YA KUTUMIA MAKEUP NI PAMOJA NA;
- Kuziba kwa vitundu vidogo vya hewa ndani ya ngozi, hali ambayo hupelekea ngozi kushindwa kupumua,kuruhusu hewa kupita, kupelekea kutokea kwa chunusi,viuvimbe n.k
- Kuharibika kwa seli za ngozi kwa urahisi zaidi hasa baada ya kuchomwa na jua,na kusababisha makunyanzi kwenye ngozi ya uso,kuzunguka macho n.k
- Matumizi ya baadhi ya makeup huongeza tatizo la ngozi kukauka kupita kawaida
- Matumizi ya baadhi ya makeup huongeza uzalishaji wa kiwango kikubwa cha mafuta kwenye ngozi na kuongeza tatizo kwa mtu ambaye ana ngozi yenye asili ya mafuta mengi
- Matumizi ya makeup huweza kusababisha tatizo la ngozi kupasuka yenyewe
- Matumizi ya makeup huweza kusababisha tatizo la Allergy ya kwenye Ngozi
- Watu wengi ambao hutumia makeup halafu wakalala nayo, huwa katika hatari ya ngozi kuharibiwa ikiwa ni pamoja na COLLAGEN kuharibika pamoja na Ngozi kubadilika RANGI yake
- Matumizi ya makeup huongeza uwezekano wa mtu kupata maambukizi ya magonjwa kwenye macho yaani Eye infection
- Matumizi ya makeup huongeza uwezekano wa mtu kupata KANSA ya ngozi
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!