UJAUZITO
• • • • • •
Nini hutokea unapokunywa pombe wakati wa Ujauzito?
Pombe ni sumu kwa mtoto. Unapokunywa pombe inaingia moja kwa moja kwenye mzunguko wa damu wa mama kasha hufika kwa mtoto kwa kupitia kondo la nyuma (placenta).
Mara pombe inapoingia kwenye mzunguko wa damu wa mtoto, huathiri uwezo wa mtoto kupata chakula, virutubisho na oksijeni ya kutosha kwa ajili ya maendeleo ya kawaida katika ubongo na viungo vingine. Hii inaweza kuathiri ubongo wa mtoto na ukuwaji wa viungo vya mwili kwa ujumla. Uharibifu huu unaweza kuathiri uwezo wa mtoto kujifunza na kufikiri pindi anapozaliwa hali ambayo itajionesha kwa matendo yake kama mtoto na kama mtu mzima.
Aidha, utafiti umeonesha kwamba uwezo wa mimba kustahimili kiwango cha pombe ni mdogo mno hali ambayop huathiri ufanyikaji wa viungo na ukuwaji wake kwa kiasi kikubwa.
Kwa kiasi gani mtoto wako ambaye hajazaliwa anaweza kuathiriwa na pombe?
Kiwango cha kuathirika kwa mimba kutokana na unywaji pombe unaofanywa na mama mjamzito hutegemea sana mambo makuu matatu ambayo ni:
Kiasi cha unywaji wa pombe
hatua ya mimba yaani umri wa mimba
mara ngapi unakunywa pombe
Matatizo yatokanayo na unywaji wa pombe
Baadhi ya madhara yanayoweza kumpata kiumbe aliye tumboni kwa mama kutokana na unywaji wa pombe kipindi cha ujauzito ni pamoja na
Kutoka/kuharibika kwa mimba
Mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo
Mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa mbavu na kidari (sternum)
Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya mgongo uliopinda (kibiongo) na vidole vilivyoundana
Mtoto kuzaliwa akiwa na kichwa kidogo kuliko kawaida (microcephaly)
Mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya pua
Kuzaliwa na matatizo ya taya
Mtoto kuwa na matatizo ya kutokuona mbali
Matatizo ya moyo kama vile moyo kuwa na tundu
Matatizo ya figo
Mtoto kuwa na ubongo mdogo na pia matatizo ya akili
Mtoto kuzaliwa akiwa na mdomo sungura (lip palate na cleft palate)
Matatizo ya kimaumbile ya masikio na ulemavu kwenye sehemu za uzazi (genital malformations).
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!