Ticker

6/recent/ticker-posts

Tatizo la kushuka kwa Kizazi,chanzo,dalili,madhara na Tiba



    UZAZI

• • • • •

Tatizo la kushuka kwa Kizazi,chanzo,dalili,madhara na Tiba


Lijue tatizo la kushuka kwa kizazi na madhara yake


Asilimia kubwa ya wanawake ambao hupatwa na tatizo la kushuka kwa kizazi, hutalikiwa na waume zao ama hutelekezwa, huku wanaume wengi wakiamini kuwa tatizo hilo linatokana na laana ambayo mwanamke hupata kutoka kwenye mizimu.


Kushuka kwa kizazi kitaalamu

Nyonga ya mamalia imeumbwa kwa mifupa madhubuti na nyama ambazo zinazunguka kiuno, nyonga imehifadhi viungo mbalimbali vya muhimu ikiwemo kizazi, kibofu cha mkojo pamoja na muishilio wa utumbo mkubwa.


Soma: Tatizo la Uke Kujamba


Katika nyonga kuna kitu mithili ya sakafu iliyotengenezwa kwa misuli, kazi yake kubwa ni kutenganisha sehemu ya juu na chini, upande wa juu ukiwa umehifadhiwa viungo mbalimbali kama kibofu cha mkojo pamoja na kizazi huku upande wa chini ukihifadhi uke pamoja na njia ya haja kubwa.


Inapotokea mushkeli katika sakafu hiyo ilioundwa kwa misuli itayosababisha hitilafu mbalimbali ambapo matokeo yake ni kulegea kwa misuli hiyo basi viungo vilivyo kwenye nyonga vinaweza kushuka ikiwemo kizazi, kibofu cha mkojo, ama utumbo wa njia ya haja kubwa au vyote kwa pamoja.


 Daktari James Chapa wa hospitali ya CCBRT anasema kuwa kushuka kwa kizazi kunatofautiana

"Wapo wananwake ambao shingo ya kizazi tu ndio inashuka lakini wapo wengine ambao hushuka kizazi chote, na kinashuka kwa namna tofauti kinaweza kushuka kuishia ndani ukeni au kikashuka hadi nje kabisa ya uke”


CHANZO;


Sababu za kushuka kwa kizazi

Katika hili wataalamu bingwa wa magonjwa ya wanawake wanathibitisha kuwa tatizo la kushuka kwa kizazi pia linaweza kusababishwa endapo mgonjwa atakuwa anatoa haja kubwa ilio kavu kuliko kawaida,


 itamlazimu kuisukuma kwa nguvu zaidi ambapo matokeo yake ni misuli ya nyonga kupata mkandamizo, unaosababisha misuli hiyo kulegea na hatimaye huenda kizazi kikashuka.


Kikohozi cha muda mrefu kisichopata tiba kinaweza kusababisha pia mtu kushuka kwa kizazi, 


kadhalika kunyanyua vitu vizito kunakojirudia tena kwa muda mrefu kunapeleka msukumo wa kishindo katika nyonga ambapo huenda misuli ikalegea na viungo kushuka ikiwemo kizazi.


Kushuka kwa kizazi si tu kwa wananwake ambao tayari wamekwisha zaa lakini pia tatizo hili linawakabili hata wale ambao hawajazaa kutokana na sababu za kijenetiki.


Aliongeza kuwa umri kwa kiwango fulani pia huchangia mwananmke kupata tatizo hili, hasa wale ambao wamekoma hedhi kutokana na mwili kushindwa kuzalisha kichocheo cha Estorogeni ambacho kazi yake kubwa ni kuifanya ile misuli iwe imara.


Wagonjwa wenyewe hawalijui tatizo la kushuka kwa kizazi.

Tatizo hili linatajwa kuwakabili wanawake tu,kutokana na maumbile yao ya uzazi yalivyo ni tofauti na wanaume, na baadhi wanapokumbwa na tatizo hili hujikuta wakijifungia kwenye dunia ya peke yao kwa kuogopa aibu na hata kusemwa na kuchukuliwa mifano katika jamii yake.


Kwa wanawake walio mijini wao hupata fursa ya kuhudhuria kliniki kipindi cha ujauzito hivyo tahadhari kama hizi huhabarishwa na wahudumu wa afya lakini,

 Kundi ambalo lipo vijijini ni nadra kupata wasaa kama huu kutokana na baadhi yao hawahudhurii kabisa cliniki au huhudhuria chini ya wastani.


MADHARA;


Madhara ya kushuka kwa kizazi kwa mgonjwa

Madhara ya kifo yanaweza kushuhudiwa kwa mgonjwa ikiwa tu hakuna uzingatiwaji wa matibabu tangu mama apatwe na tatizo hilo, kutokana na kushuka kwa kizazi kunaweza kusababisha kutofanya kazi kwa viungo vingine ikiwemo figo,


 lakini madhara mengine ni kupata maamukizi kwenye kizazi kutokana na kizazi kuwa nje muda wote.


Baadhi ya wagonjwa wanaokabiliwa na tatizo la kushuka kwa kizazi wengine huzikimbia kabisa ndoa zao na wengine huachwa ama hutelekezwa na waume au wenza wao, hii ni kutokana na tatizo hilo kuhusishwa na imani za kishirikina.


Tatizo hili wamelifanya kuwa ni la siri sana ndio maana wanajikuta wapo peke yao, wamelihusisha na imani za kishirikina kwakiasi kikubwa, na pia hawapendi kufanya tendo la ndoa kutokana na maumivu makali wanayoyahisi.”


MATIBABU;


Matibabu ya kushuka kwa kizazi

Katika kumsaidia mgonjwa kupata matibabu katika tatizo la kushuka kwa kizazi,


 matibabu yamegawanyika katika makundi mawili wapo ambao watapatiwa tiba ya mazoezi hasa ya nyonga ili kurejesha misuli katika ukakamavu unaotakiwa na mwili na hatimae kizazi kurejea katika sehemu yake.


Kadhalika lipo Kundi la wanawake ambao wanawekewa vifaa maalum ambavyo kitaalamu vinaitwa "Pesars”  ni vimipira maalumu ambavyo vinaukubwa tofauti kulingana na ukubwa wa maumbile ya mgonjwa ambapo kazi kumbwa vinafanya kurudisha kizazi sehemu yake,


Matibabu ya mwisho kabisa yakiwa ni upasuaji na kurekebisha sehemu ambayo inahitilafu ili kumrejeshea mama furaha yake

"Katika upasuaji tunachozingatia ni kama mama amekoma kuzaa basi tunatoa kabisa kizazi, lakini kama bado yupo kwenye rika la kuzaa tunazingatia kurudisha kizazi katika eneo lake linalostahili kukaa na atarudi kama zamani


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments