CHANZO CHA HASIRA KWA MWANAMKE WAKATI WA SIKU ZA HEDHI

HEDHI

• • • • • •

CHANZO CHA HASIRA KWA MWANAMKE WAKATI WA SIKU ZA HEDHI


Bila shaka utakuwa shahidi au hata wewe mwenyewe ni mhusika kwamba kwa baadhi ya wanawake  wakiwa kwenye siku zao za hedhi(menstrual period) huwa na Hasira sana kupita kawaida, je chanzo cha shida hii ni nini?


CHANZO CHAKE NI NINI?


Ukweli ni kwamba mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo imehusishwa kwenye hili la mwanamke kuwa na Hasira sana wakati wa siku za hedhi japo baadhi ya tafiti na majarida mbali mbali ya afya yamehusisha na sababu hizi hapa chini;


• Mabadiliko ya vichocheo au hormones ambayo hutokea wakati wa hedhi, na mabadilko hayo huhusisha vichocheo vikubwa viwili ESTROGEN pamoja na PROGESTERONE ambapo huleta matokeo mpaka kwenye mood ya mtu,


Wakati yai la mwanamke linatoka kwenye vifuko vya mayai yaani ovaries kiwango cha hormone ya ESTROGEN pamoja na PROGESTERONE hushuka sana hali ambayo huweza kupelekea kupungua pia kwa kiwango cha SEROTONIN kwenye mwili wako,


Kushuka kwa kiwango cha Serotonin mwilini huleta matokeo mbali mbali kwenye mwili wako kama vile;


- Mwanamke kuwa na Hasira sana


- Mwanamke Kushindwa kutulia na kufanya kitu kimoja


- Mwanamke kuwa na tatizo la kukosa kabsa Usingizi, utakuwa shahidi kwamba wanawake wengi hukosa usingizi wakiwa kwenye kipindi cha hedhi


- Mwanamke kuhisi huzuni sana


- Mwanamke kuanza kuchagua baadhi ya vyakula na kuchukia vingine n.k


JINSI YA KUDHIBITI HALI YA HASIRA SANA UKIWA KWENYE SIKU ZA HEDHI


Zoezi hili la kuweza kudhibiti hasira wakati wa siku za hedhi kwa mwanamke sio la siku moja,linahitaji muda pamoja na mazoezi ya kila mara, na kujua njia gani sahihi inafanya kazi kwako vizuri zaidi kwani njia zipo zaidi ya moja na wanawake wanatofautiana.


Unashauriwa kuanza kuweka kumbukumbu ya Tarehe kwa kila mzunguko wa hedhi ambapo hasira huanza kujitokeza,hii itakusaidia sana wakati wa kudeal na hili tatizo la hasira wakati wa hedhi,kisha baada ya kujua hizo tarehe kwenye mizunguko mbali mbali ya hedhi fanya mambo haya hapa chini;


• Epuka vitu vyote ambavyo vinakufanya usitulie au kukuletea msongo wa mawazo


• Refresh mind kwa vitu vyepesi zaidi,epuka kazi nyingi sana pamoja na kutoka out kama unapenda


• Fanya mazoezi ya mwili,njia hii husaidia sana kwa kiwango kikubwa


• Kula vyakula unavyovipenda sana


• Pata muda mzuri wa kulala usiku N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!