CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI SANA YA TUMBO WAKATI WA HEDHI(dysmenorrhea)

HEDHI

• • • • • 

CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI SANA YA TUMBO WAKATI WA HEDHI(dysmenorrhea)


Wanawake wengi husumbuliwa na tatizo la maumivu makali sana ya tumbo wakati wa hedhi hadi wengine kufikia hatua ya kushindwa kufanya chochote na kulazwa hospitalini, Je chanzo cha tatizo hili ni nini? Endelea kusoma makala hili ili ujifunze zaidi.


 Kwanza kabsa tuanze na dalili za tatizo la maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi.


Dalili za maumivu ya tumbo wakati wa Hedhi ni pamoja na:


✓ Mwanamke Kupata maumivu makali ya tumbo mithili ya mtu anakuminya,kukugandamiza au kukatwa na kitu kikali chini ya kitovu chako


✓ Maumivu ambayo huanza siku 1 hadi 3 kabla ya kipindi chako cha hedhi, hufikia masaa 24 baada ya kuanza kwa kipindi chako na hupungua kwa siku 2 hadi 3


 ✓ Maumivu ambayo husambaa nyuma ya mgongo,kiunoni na kwenye mapaja


 ✓ Wanawake wengine pia hupatwa na tatizo la:


 i). Kichefuchefu na kutapika


 ii). Maumivu ya kichwa


iii). Kizunguzungu 


iv). Kuharisha n.k


 CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI SANA YA TUMBO WAKATI WA HEDHI(wanawake)

 

 Wakati wa hedhi, tumbo la uzazi yaani UTERUS hugandamizwa zaidi na kusinyaa(contract) mithili ya kukamuliwa ili kutoa nje uchafu ambao hauhitajiki tena, sasa wakati mchakato huu unafanyika ndipo tatizo la kupata maumivu ya tumbo huanzia hapo.


Dutu zinazofanana na vichocheo au homoni za prostaglandini ndizo zinazohusika na kusababisha maumivu,mgandamizo na uchochezi zaidi ili kutoa uchafu ambao hauhitajiki tena ndani ya mji wa mimba.


Sasa basi uzalishwaji wa vichocheo hivi vya Prostaglandins ambavyo huhusika katika mchakato mzima wa kuleta maumivu na mgandamizo ndani ya kuta na misuli ya mji wa mimba(uterus) hutofautiana kiwango kati ya Mwanamke mmoja na mwingine.


Endapo Prostaglandins zimezalishwa kwa kiwango kidogo sana mwanamke hupata maumivu kidogo lakini endapo zimezalishwa kwa kiwango kikubwa sana mwilini na mwanamke hupatwa na maumivu makali zaidi.


Na zipo sababu mbali mbali za kutokea kwa mabadiliko hayo na mwanamke kupata maumivu makali sana ya tumbo wakati wa hedhi,na sababu hizo ni kama vile;

 

1. Tatizo la Endometriosis, ambapo kuta za ndani ya mji wa mimba huvimba hali ambayo hupelekea kuta hizo kutokeza kwa nje hasa kwenye maeneo kama vile; kwenye mirija ya uzazi yaani Fallopian tubes, kwenye vifuko vya mayai yaani Ovaries, au kwenye tishu zinazofunika mfupa wa nyonga yaani Pelvis.


 2. Tatizo la Uvimbe kwenye kizazi(Fibroids),  Uvimbe kwenye kizazi huweza kusababisha tatizo la maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi.


 3. Tatizo la Adenomyosis, ambapo Tishu zinazofunika tumbo lako la uzazi yaani uterus huanza kukua ndani ya kuta za misuli ya uterasi.


4. Ugonjwa wa PID(pelvic inflammatory disease) ukiwa na maana ya maambukizi ya bacteria kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke

 

wanawake wenye PID huweza kukumbwa pia na tatizo la maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi hadi wengine kushindwa kufanya chochote na kulazwa hospitalini.


 5. Tatizo la Cervical Stenosis, Kwa wanawake wengine, mlango wa kizazi yaani CERVIX huwa ni mdogo sana hali ambayo husababisha shinikizo zaidi na mgandamizo mkubwa wakati uchafu(Hedhi) ukitolewa nje kutoka kwenye kizazi. Shinikizo hili huongeza maumivu zaidi ya tumbo wakati wa hedhi

 

WANAWAKE AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO WAKATI WA HEDHI NI PAMOJA NA;

 

 • Wanawake wenye umri mdogo chini ya miaka 30


 • Wanawake wanaoshambuliwa na magonjwa kama PID mara kwa mara


• Wanawake wanaowahi kubalehe au wanaobalehe mapema, kati ya umri wa miaka 11 au chini


• Wanawake wanaovuja damu nyingi wakati wa hedhi

 

 • Wanawake wenye mzunguko wa hedhi usio na tarehe maalumu(wenye kubadilika badilika) yaani irregular menstrual cycle


• Wanawake waliopo kwenye familia ambazo zina historia ya watoto wa kike kupata maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi (dysmenorrhea)


 • Wanawake wanaovuta sigara n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!