MIGUU
• • • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA KUKAZA MISULI YA MIGUUNI
Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia kutokea kwa tatizo hili kama vile;
• upungufu wa maji mwilini, ambao hutokana na sababu mbali mbali kama vile kutokunywa maji ya kutosha n.k
• kufanya kazi zinazohusisha miguu kwa kiasi kikubwa,kutembea umbali mrefu au michezo kama mpira wa miguu huweza kuchangia tatizo la kukaza kwa misuli ya miguuni
• Tatizo la kuwa na mzunguko mbaya wa damu(poor blood flow) kwenye mishipa na misuli ya miguuni. Kupungua kwa mishipa ambayo husafirisha damu kwenye miguu yako (arteriosclerosis) huweza kusababisha maumivu pamoja na misuli ya miguu kukaza sana,
japo shida hii huondoka mara tu baada ya kuacha kufanya mazoezi kama tatizo limetokea wakati wa kufanya mazoezi.
• Ukandamizaji wa neva pamoja na mishipa ya damu mgongoni. Ukandamizaji wa mishipa kwenye mgongo wako (lumbar stenosis) pia inaweza kusababisha maumivu pamoja na kukaza kwa misuli ya miguuni.
Maumivu haya huzidi sana wakati unatembea.
• Kupungua kwa madini mwilini kama vile; Potasiamu, kalsiamu au magnesiamu katika lishe yako inaweza kuchangia maumivu ya miguu pamoja na tatizo la misuli kukaza.
• Matumizi ya dawa jamii ya Diuretics - dawa hizi huweza kuchangia mtu kutoa maji mengi mwilini kwa njia ya Mkojo,kuathiri mzunguko wa damu(shinikizo la damu) pamoja na upungufu wa madini kama potassium,magnessium,calcium n.k.
MAKUNDI YA WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATWA NA TATIZO HILI LA KUKAZA KWA MISULI YA MIGUUNI
✓ Wazee(Umri)- Wazee hupoteza misuli, kwa hivyo misuli iliyobaki inaweza kuzidiwa kwa urahisi zaidi.
✓ Wanariadha pamoja na wanamichezo wengine kama vile wachezaji wa Mpira wa Miguu ambao wamechoka na kukosa maji mwilini wakati wanashiriki kwenye michezo majira ya hali ya hewa ya joto mara nyingi huwa na tatizo hilo la misuli ya miguuni kukaza.
✓ Wajawazito- Uvimbe wa misuli,maumivu pamoja na kukaza ni kawaida sana wakati wa ujauzito.
JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI
- Kunywa maji ya kutosha,angalau lita 2.5 mpaka 3 kwa siku
- Nyosha misuli yako. Nyoosha kabla na baada ya kutumia misuli yoyote kwa muda mrefu. Ikiwa huwa na maumivu ya miguu usiku, nyoosha kabla ya kwenda kulala. Mazoezi mepesi, kama vile kuendesha baiskeli iliyosimama kwa dakika chache kabla ya kwenda kulala, pia inaweza kusaidia kuzuia tatizo hili wakati umelala.
Hata hivo kwa asilimia kubwa kukaza kwa misuli ya miguuni hakuna madhara makubwa kwani hutokea kwa muda mfupi na kuachia,
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!