Ticker

6/recent/ticker-posts

CHANZO CHA TATIZO LA KUTOKWA NA MBEGU ZA KIUME(SHAHAWA) UUME UKIWA HAUJASIMAMA



 AFYA YA UZAZI KWA WANAUME

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA KUTOKWA NA MBEGU ZA KIUME(SHAHAWA) UUME UKIWA HAUJASIMAMA


Tatizo la kutokwa na sperm/mbegu za kiume/semen au shahawa wakati hufanyi mapenzi au uume ukiwa haujasimama ni tatizo ambalo linatokea kwa baadhi ya wanaume. je chanzo cha tatizo hili ni nini?


Katika hali ya kawaida wanaume hutoa shahawa au maji maji kwenye uume wakati wanajiandaa kufanya tendo la ndoa, wakati wanafanya tendo la ndoa, wakati wapo kwenye hisia za kimapenzi, wakati wanapiga punyeto au masturbation n.k


Lakini kuna baadhi ya wanaume hupatwa na tatizo la kutokwa na maji maji kwenye uume(semen) kama yale wakati mtu akiwa katika hisia kali za kimapenzi au wengine humwaga kabsa shahawa wakati uume haujasimama, hawapo kwenye hisia za kimapenzi, wapo tu wamekaa katika hali isio na viashiria vyovyote vya kimapenzi.


CHANZO CHA TATIZO LA KUTOKWA NA MBEGU ZA KIUME(SHAHAWA) UUME UKIWA HAUJASIMAMA AU WAKATI HAUPO KWENYE HISIA ZOZOTE ZA KIMAPENZI


1. Wakati umelala, Wanaume wengi wakati wamelala huweza kuota ndoto ambazo hujulikana kama wet dreams au Nocturnal emissions, hali ambayo hupelekea kujiona wanafanya mapenzi kisha kumwaga shahawa, hii hutokea sana wavulana wakiwa katika kipindi cha ukuaji yaani Balehe au Puberty


MATIBABU

Katika hali ya kawaida huhitaji matibabu yoyote kama chanzo cha tatizo lako ni hiki hapa.


2. Matumizi ya baadhi ya dawa; dawa jamii ya ANTIDEPRESSANTS huweza kusababisha matatizo mbali mbali mwilini kama vile;

- mbegu za kiume kutoka nje ya uume au mwanaume kumwaga shahawa wakati hafanyi mapenzi wala hayupo kwenye mazingira hayo

- Mwanaume kukosa kabsa hamu ya tendo la ndoa

- Mwanaume kuchelewa sana kufika kileleni

- Mwanaume kuwa na tatizo la  upungufu wa nguvu za kiume,uume kushindwa kusimama au kwa kitaalam Erectile dysfunction

• Dawa zingine ni kama vile mood stabilizers au baadhi ya dawa za kutibu matatizo ya hormones mwilini

MATIBABU

Ukiona dalili hizi za kutoa shahawa wakati haupo kwenye mazingira ya kufanya tendo la ndoa halafu unatumia dawa katika makundi hayo hapo juu niliyoeleza,unashauriwa kuongea na daktari wako ili ikiwezekana ubadilishiwe dawa na kuacha dawa hizo.


3. Matatizo kwenye tezi la PROSTATE, Tezi la Prostate husaidia kutoa SEMEN ambazo ndizo hufanya kazi ya kusaidia kusafirisha mbegu za kiume kutoka kwenye uume,tezi hili huweza kukumbwa na matatizo mbali mbali kama vile;

- Kuvimba kwa tezi au kuongezeka ukubwa yaani Prostatitis kutokana na sababu mbali mbali kama vile maambukizi ya bacteria,matatizo kwenye mfumo wa kinga ya mwili,tatizo la kansa au Saratani n.k

Unashauriwa kuwahi hospitalini endapo utaona dalili hizi hapa chini;


• Kupatwa na maumivu ya mkojo wakati wa kukojoa

• Kutoa mkojo ambao umechanganyika na damu

• kutoa shahawa ambazo zimechanganyika na damu

• Kushindwa kufika kileleni kwa haraka,kushindwa kabsa kufika kileleni au kuwahi sana kuliko kawaida,uume kushindwa kusimama n.k

• Kupata maumivu makali wakati unafika kileleni


MATIBABU

Matatizo ya tezi la Prostate huhusisha tiba mbali mbali kulingana na chanzo chake kama vile huduma ya upasuaji na kuondolewa kwa tezi hilo pamoja na tiba zingine.


4. Tatizo la kwenye mfumo wa nerves au Nerves Injury

Endapo mwanaume kupatwa na jeraha au tatizo lolote linaloharibu nerves au mfumo wa fahamu huweza kupatwa na matatizo mengine mbali mbali kama vile;

- Hili la kutoa mbegu za kiume au kumwaga uume ukiwa haujasimama,ukiwa hufanyi mapenzi na wala huna hisia hizo kwa wakati huo

- Mabadiliko kwenye nguvu za kiume,uwezo wa uume kusimama, kushindwa kufika kileleni kabsa,kuchelewa au kuwahi kufika kileleni n.k

Tatizo la nerves kuharibiwa huweza kusababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo maambukizi ya bacteria,umri mkubwa,magonjwa ya zinaa, upasuaji kwenye uti wa mgongo,kuumia kwa kupata ajali n.k


MATIBABU

Matibabu ya tatizo la kuharibika kwa nerves hutegemea na chanzo chake hivo lazima uongee na wataalam wa afya kwanza,kufanya vipimo kisha kujua chanzo chake na kuanza tiba


KUMWAGA SHAHAWA BAADA YA KUKOJOA

Hili si tatizo kwani wanaume wengi hupatwa na hii hali hasa mda mfupi tu kama ndyo wametoka kufanya mapenzi, kwani baadhi ya shahawa huweza kubaki kwenye njia ya mkojo yaani Urethra hivo hutolewa nje wakati wa kukojoa,

Japo huweza kuwa tatizo endapo hali hii hutokea kila mara, na kuhusishwa na matatizo mengine kama vile maambukizi ya bacteria,kuumia kwenye nerves, magonjwa ya zinaa N.k, Hivo kama ni tatizo la kujirudia kila mara muone daktari.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments