CHANZO CHA TATIZO LA KUVUJA JASHO KUPITA KIASI KWENYE KWAPA

 JASHO

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA KUVUJA JASHO KUPITA KIASI KWENYE KWAPA


Katika hali ya kawaida kuvuja jasho ni mojawapo ya mifumo ya mwili katika kutoa taka mwili nje na kukufanya uwe na afya zaidi, jasho huweza kutoka kwenye maeneo mbali mbali ya ngozi yako kama vile; Usoni, kwenye kwapa, tumboni,kwenye mikunjo ya miguuni,mikononi,shingoni au mwili mzima.


Na kutokwa na jasho mwilini kwa kawaida huweza kusababishwa na hali mbali mbali kama vile; jua kali,joto kali,mtu kufanya mazoezi mbali mbali n.k


Lakini endapo unatoa jasho jingi sana kwenye maeneo kama KWAPANI bila kuwa na chanzo chochote cha joto huweza kuwa ni tatizo ambalo huhitaji Tiba.


Kuna baadhi ya Watu husumbuliwa na tatizo la kuvuja jasho jingi sana kwapani bila kujali kuna baridi au joto,bila kujali wapo kwenye jua au kivulini,bila kujali wamevaa nguo nyingi nzito au hawajavaa, je nini huweza kuwa chanzo cha tatizo hili?


HIZI HAPA NI BAADHI YA SABABU ZA MTU KUVUJA JASHO JINGI KWAPANI


1. Mtu kuwa na tatizo la Shambulio la moyo yaani Heart attack


2. Mtu kuwa na tatizo la kisukari ikiwa ni pamoja na sukari kuwa chini sana kwenye damu yaani Low Blood sugar


3. Mtu kuwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile FANGASI wa kwapani n.k


4. Mtu kuwa na Matatizo mbali mbali katika mfumo wa fahamu au Nerves system


5. Dalili za mwanamke kufikia kwenye kipindi cha Ukomo wa Hedhi yaani Menopausal hot flashes


6. Mtu kuwa na matatizo ya baadhi ya Kansa au Saratani kama vile Kansa ya ngozi n.k


7. Mtu kuwa na matatizo kwenye Tezi la THYROID n.k


Hizo hapo juu ni baadhi ya Sababu ambazo huweza kuchangia mtu kuwa na tatizo la kuvuja jasho kwapani kupita kiasi, Hivo ukiona hivo wasiliana na Wataalam wa afya kwa ajili ya kupata matibabu.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!