magonjwa
DALILI ZA TATIZO LA DAMU KUGANDA
Imeboreshwa July 10, 2026 by Doctor Ombeni
DAMU KUGANDA
• • • • • •
DALILI ZA TATIZO LA DAMU KUGANDA
Dalili za tatizo la damu kuganda huweza kuonekana kwenye maeneo mbali mbali ya mwili kama vile mikononi,miguuni, kwenye mapafu, kwenye moyo n.k
Wakati damu imeganda(Blood clots) kwenye mishipa ya vein miguuni au mikononi hali ambayo hujulikana kwa kitaalam kama deep vein thrombosis (DVT) ni hatari kwani clots za damu huweza kusafiri moja kwa moja kwenda kwenye moyo au mapafu.
Na sana sana damu kuganda maeneo kama haya hutokana na mtu kukaa sehemu moja kwa muda mrefu,kutokutembea kwa sababu mbali mbali kama vile ugonjwa wa miguu, upasuaji n.k
DALILI ZA TATIZO LA DAMU KUGANDA
1). Miguuni au Mikononi
– Mikono au miguu kuvimba na hii huanza kuonekana pale tu damu inapoanza kuganda
– Rangi ya ngozi mikononi au miguuni kubadilika na kuwa Nyekundu zaidi au Blue, na baadhi ya watu huanza kupatwa na miwasho ya ngozi maeneo haya
– Maumivu ya miguu au mikono ambayo huongezeka kadri siku zinavyosogea mbele
– Ngozi ya sehemu ambapo damu imeganda au tatizo la deep vein thrombosis (DVT) limetokea huwa ya moto zaidi kuliko sehemu zingine
– Misuli ya miguu kuanza kukakamaa(lower leg muscle cramps)
– Uvimbe miguuni ambao huambatana na maumivu ya miguu n.k
2). Mapafu
Kama zile clots za damu baada ya kuganda zimefika kwenye mapafu hali ambayo hujulikana kama pulmonary embolism ni hatari sana kwa mgonjwa, na mgonjwa huweza kuanza kupata dalili hizi hapa;
– Kupata shida sana ya kupumua au kukosa hewa
– Mgonjwa kuanza kukohoa sana, wengine hukohoa hadi damu
– Kuanza kupata maumivu makali ya kifua wakati wa kupumua
– Kupatwa na kizunguzungu kikali
– Kutokwa na jasho sana mwilini n.k
3). Moyo
– Mgonjwa kupata maumivu makali ya kifua pamoja na mikono
– Mgonjwa kutokwa sana na jasho mwilini
– Kupata shida wakati wa kupumua au kupumua kwa shida
– Kuwa katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo yaani Heart attack
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
-
magonjwa2 years ago
Muwasho sehemu za siri kwa mwanaume chanzo chake
-
jinsi ya kupunguza tumbo2 years ago
Mbinu za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka
-
Afya ya mtoto2 years agoMambo ya kuzingatia kwenye utunzaji wa Kitovu cha Mtoto mchanga
-
Madhara ya mtoto kunywa maji machafu4 weeks agoMadhara ya mtoto kunywa maji machafu au maji ya uzazi
-
Madhara ya Pombe3 weeks agoJE, POMBE hupunguza testosterone na Ubora wa mbegu za Kiume?
-
afya5 years agoCHANZO CHA TATIZO LA KUPASUKA MIGUU KWENYE KISIGINO(gaga)
-
uzazi1 week agoVyakula vya kuongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha
-
afya5 years agoFAHAMU KUHUSU VIRUSI VYA CORONA NA UGONJWA WA COVID 19(chanzo,dalili,madhara,tiba)



